CHE GUEVARA-II
JF-Expert Member
- Jun 17, 2010
- 571
- 156
Wadau naomba kupata ukweli juu ya hii miti ya mitiki,kuna mengi yanasemwa juu ya miti hii,kifupi mimi naomba kujua,je ni 1: kweli kua miti hii ni ghali sana kidunia? 2: ni kweli kua zipo baadhi ya banks hapa nchini zinatoa mikopo ukiwa na miti hii?kama ni kweli je ni bank gani hizo? 3:je mitiki uwa inachukua muda gani kuanza kukua mpaka kufikia hatua ya kuingizwa sokoni?kuna mtu aligusia kua kuna aina tofauti tofauti za miteak na ukuaji wake,ila nae hana uhakika sana juu ya ilo
Wakuu, mimi mwenyewe nasubiri majibu ya kiundani zaidi kuhusu hiki kilimo cha mitiki.
Nataka nianze mchakato 2014, ili by 2035 nikiwa NIMESHAKUFA (au nikiwa bado niko hai at 60's) mwanangu aliye na miaka 3 sasa atakuwa ana 25 yrs (akiwa Chuo Kikuu akisomea masuala ya Public Administration, Bussiness Administration na/ au mambo mengine yanayofanana na hayo) ili akimaliza Chuo kikuu atumie hizo billioni kadhaa zitakazo kuwa zimetokana na mitiki kusimamia kazi zake kwa kuhakikisha anaajiri wataalamu watakaoendesha miradi yake kwa ufanisi.
.....Maige alisema wakati mahitaji ya mbao nchini kwa mwaka yanafikia meta za mraba milioni tano, uwezo wa mashamba yaliyopo ni kuzalisha meta za mraba milioni 1.5 tu. Alisema Sh milioni 40 zinatosha kuhudumia ekari moja ya shamba la mitiki kwa miaka 20, lakini mazao yake yakazalisha zaidi ya Sh bilioni 3. .......
Reference (March 2012): MOROGORO FAMILY - MOROGORO YETU: TANAPA 'YALIWA' KWENYE MAGOGO YA MITIKI.