Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

mkuu kisima na wengine nimepata kufuatilia nyuzi karibia zote na kupata maelezo toshelezi kuhusu kilimo cha miti
nami ni kijana hata robo karne sijafikisha nikaona si mbaya nami nikajaribu kuwekeza japo kwa mchanganyiko wa miti ile ya muda mfupi na ya muda mrefu kama mitiki
sasa basi kwakua mimi mtaji ni mdogo na sina shamba tatizo lipo hapa
Wapi naweza pata shamba kuanzia ekari tano kwa bei nafuu zaidi kutoka kwa kijiji hasa mikoa ya Tanga,iringa, na morogoro.?
Miti gani ni yenye faida na soko ya muda mfupi means 10 down to 7?
Misimu ya upandaji na bei za mbegu na upatikanaj wake
shukran mkinisaidia kwa hili wakuu
 
katika mbegu ambazo ninaweza kuziandaa ni za mitiki hadi kupanda kitaluni

Mbegu zote unaweza kuandaa kama unao muda wa kutosha.
Kuhusu mashamba inategemea na sehemu husika ila kwa Moro&Tanga(mitiki) changamoto kubwa ni wafugaji tu bei iko chini. Kwa syprus nenda Iringa au Sengerema ila changamoto ni upatikanaji wa eneo kubwa mahala pamoja na bei ipo juu sana.
 

nimekupata brother
 
Mkuu kisima..hapo Moro uko maeneo gani?na kama hutojali naweza pata eneo la bei rahisi kwa kilimo na ufugaji...

Pole sana mkuu nimechelewa kujibu kutokana na sababu zilizo inje ya uwezo wangu!
Mi napatikana Turiani, maeneo/shamba kwajili ya kilimo na ufugaji yanapatikana sana tu. Mhimu ni kujua unataka eneo lenye sifa zipi ili kurahisisha shughuri zako za kilimo.
Je, liwe na chanzo cha maji? Barabarani? Bonde? Mlima etc na bei inatofautiana kulingana na sifa ya shamba.
Nakuomba tuwasiliane kwa maelezo zaidi.
 
Mkuu Kilimo mitiki inastawi ukanda wote wa pwani, kwa mikoa ya pwani, moro na tanga ndipo mahala pake haswaa kwa upandaji wa mitiki. Maeneo ya baridi kali mitiki haikui haraka na hudumaa.

Ahsante sana mkuu nilikuwa natafuta sana knowledge ya hii miti nataka nipande takribani miti elfu kumi ngoja nikanunue ardhi kwa ajili ya hii miti.
 
Last edited by a moderator:
15+ yrs mkuu, kama umeamua kujikita kwenye kilimo cha miti nakushauri upande na pines, cyprus, msila etc hii inavunwa mapema kuliko mitiki, japo mitiki ni habari nyingine interms of thamani.

Hizo species za pines,cyprus na msila miche yake inauzwaje na inachukua muda gani kuwa tayari kwa kuvunwa.
 
Hizo ni ndani ya miaka kumi mkuu unalamba hela, cyprus&pine ni tsh50k kwa chupa ya ml350 zipo punje zaidi ya 2k ntakupa njia ya kuziandaa kwajl ya kuweka kitaru.
Msila debe1 la mbegu ni sh50k.
 
Hizo ni ndani ya miaka kumi mkuu unalamba hela, cyprus&pine ni tsh50k kwa chupa ya ml350 zipo punje zaidi ya 2k ntakupa njia ya kuziandaa kwajl ya kuweka kitaru.
Msila debe1 la mbegu ni sh50k.

Shukrani sana mkuu.
 

Kisima naomba mawasiliano yako nataka miche ya mitiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…