Kilimo cha mpunga Tanzania

Sehemu nyingi za morogoro huwa hawalindii ndege mashambani kwa sababu , mipunga mingi inakuwa imekwiva kwa hiyo swala la ndege linakuwa hadidhi unaweza kuta sehemu ekali zaid ya 300 kote ni mashamba ya watu ya mpunga na wote umeiva kwa pamoja sasa hapo hakuna ndege . Kuna kilimo cha kupanda umpunga ,unapanda kama unavyopanda mahindi hiki pia huongeza kipato tofauti na kilimo cha kumwaga mbegu,
 



BIG UP SANA mkuu. Mimi ndio nimeagiza hiyo planter natumaini nitaanza kuitumia kuanzia msimu ujao. Msimu huu inachelewa kufika
 
Mpunga sikuhizi kyela hakuna kitu ns usangu wanaweka mbolea na madawa mpunga mzuri ni wa kamsamba rukwa huo ndo super kwa sasa ni mtamu na unanukia balaa na kule hawaruhusu mbolea mashambani mwao
mpunga Ni biashara, ili kuongeza kipato hakuna mpunga usiopigwa mbolea. Watu wako radhi kupiga mbolea usiku wa manane
 
Kuna kile kilimo cha umwagiliaji ambapo unaweza vuna mwezi wa tano na June ukapanda tena ukavuna November.
Nipe tofauti ya uvunaji wake .
 
Kuna kile kilimo cha umwagiliaji ambapo unaweza vuna mwezi wa tano na June ukapanda tena ukavuna November.
Nipe tofauti ya uvunaji wake .
Mavuno huwa ni kidogo Sana tofauti na kulima wakati wa mvua. Vile vile kulima Mara mbili inawezekana iwapo utakua na chanzo Cha maji Cha uhakika.
 
Asante kwa darasa🙏
Naomba kujua zaidi upandaji wa mbegu za mpunga kwa vijembe, hasa faida zake na je ni kweli kua unaongeza kipato ukilinganisha na njia nyingine??
 
Maonyesho ya vyuo vikuu kuna chuo kimekuja na hiyo teknolojia
 
Naomba kuuliza ni Maeneo gani naweza kupata mashamba ya mpunga kukodi kwa bei rahisi
 
Naomba kuuliza ni Maeneo gani naweza kupata mashamba ya mpunga kukodi kwa bei rahisi
Bei rahisi ni morogoro, pwani, na Ruvuma. Uhakika zaidi ni morogoro na pwani maeneo mengine yanakumbwa na ukame wa Mara Kwa Mara hivyo Kama hakuna mfumo wa umwagiliaji kukaanga mtaji ni sekunde.
 
Asante kwa darasa[emoji120]
Naomba kujua zaidi upandaji wa mbegu za mpunga kwa vijembe, hasa faida zake na je ni kweli kua unaongeza kipato ukilinganisha na njia nyingine??
Njia pekee inayoongeza kipato ni upandaji wa mpunga Kwa kupandikiza Miche michanga(shadidi). Njia ya vijembe Sina utaalam nayo lakini naamini itakua ni mbadala wa usiaji(umwagaji ) wa mpunga. Kama itakua ni hivyo basi itakua na faida kuliko kumwaga kwani itatoa nafasi ya Miche kukua na kupacha lakini haiwezi kufikia kipato Cha upandaji wa kupandikiza Miche.
 
Mkuu je nikitaka kukodi heka 50 naweza kupata sehemu moja kwa mkoa wa morogoro?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…