Kilimo cha muda mfupi nafuu na kinacholipa

snochet

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
1,433
Reaction score
1,176
Nimekuwa nikitafakari kitu cha kuwekeza kwenye shamba ambaloo liko sehemu ambayo ni remote kidogo.yaani watu bado hawaishi wengi,na ningependa kufaanya kkilimo.kwa muda wa kama miezi mitatu.ninasikia kuna aaina ya maharage yanaitwa ngwara(au ngara,sina uhakika) yana bei nzuri sana hasa kwa nchi jirani ya Kenya ambayo unaweza ukauza hata kwa Tsh300,000/= kwa gunia moja la kilo mia moja.kama kuna mtu anafahamu tafadhali naomba atujuze.na kama kuna mazao mengine tusiyoyajua yenye bei nzuri tafadhali tujulishane.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Ngwara inatambaa sana hivyo inahitaji eneo kubwa. Alaf pod zake haizai zaidi ya punje tatu. Ni kweli ina bei nzuri lakini uwe na eneo kubwa
 
Lima matikiti maji km eneo lako lina upatikanaji wa maji wa uhakika kwa ajili ya umwagiliaji.

Uncle, unaweza ukachanganua kidogo kwenye hili la matikiti maji? Au kama kuna thread humu ilishawahi kuzungumzia ntashukuru kama uki post hapa.
 
Duh mdau ngwara inachukua muda mrefu kiasi kupanda hadi kuvuna, it takes about 5 months minumum. Sidhani kama hilo ni wazo zuri sana.
 
Nashukuru sana kwa mawazo yenu, je matikiti yanachukua muda gani? Na ina upandaji wa kipekee? Kama ndiyo naomba unifahamishe
 
Vipi kulima pilipili manga? Nasikia gunia moja unakula 600,000
 
Acha habari za naskia...fanya utafiti.

Kwa kuanzia nakushauri upite pale sokoni kariakoo, lile linaitwa soko la zamani au soko la nazi, tafuta mfanyabiashara ya viungo kisha muulize manga inauzwaje kwa kilo(bei ya reja reja) na yeye yupo tayari kununua kwa kiasi gani kutoka kwa mkulima(ambaye ni wewe), mueleze ukweli tu kuwa unafanya utafiti na kwamba unakusudia kulima manga. Hapo utapata picha halisi ya mambo yalivyo na si kuishi kwa naskia, naskia.

Nimewahi kupata mawazo kama yako ya kulima manga, nikatafiti wapi inastawi...niliambiwa pahala fulani ndani huko mahenge, usafiri ni wa treni ya tazara vinginevyo uwe na four wheel drive kama land rover defender au landcruiser mkonga, nilichogundua ni kuwa si jambo jepesi sana kulima spices kama manga, hiliki na mdalasini, ni changamoto kama ilivyo changamoto yetu ya kila siku ya kuamka asubuhi kwenda kazini mpaka saa 11 jioni.
 
Uncle, unaweza ukachanganua kidogo kwenye hili la matikiti maji? Au kama kuna thread humu ilishawahi kuzungumzia ntashukuru kama uki post hapa.

Matikiti, mananasi yote matatizo matupu...vijana wa hapo dar walidanganyana sana miaka kadhaa iliyopita kwamba ni fast money making ways. wakavamia mashamba kiwangwa, bunju na chanika kulima mananasi na matikiti, wengi waliambulia hasara na sasa wametambua kwanini babu zao walilima na wamekufa masikini..kilimo si kazi ya watu masikini.
 
matikiti, mananasi yote matatizo matupu...vijana wa hapo dar walidanganyana sana miaka kadhaa iliyopita kwamba ni fast money making ways. wakavamia mashamba kiwangwa, bunju na chanika kulima mananasi na matikiti, wengi waliambulia hasara na sasa wametambua kwanini babu zao walilima na wamekufa masikini..kilimo si kazi ya watu masikini.

Al Zaqawi

you have said it all, huu ushauri wako ukizingatiwa hapa jf itaweza kuwa chachu ya mabadilko ya kilimo hapa Tanzani

ukweli ni kwamba bila kuwa na mitaji mikubwa na kufanya kilimo cha technologia, kilimo kitabakia kuwa ni majaribio na shughuli ya kutafuta hela ya kula na siyo kupata faida na maendeleo
 
@ramthods, mzee kua reasonable nahisi unataka kusuggest kua kilimo hakima faida. hamna kitu rahisi duniani, hilo ndo la muhimu. otherwise, msimu uliopita mvua za vuli au short rains nimelima matikiti maji aina ya sugar baby takriban acre tano nimevuna tonne 30+..! kilo moja ya matikiti inavary between 150 to 300 depends on the market condition. matikiti yanastawi zaidi kwenye ardhi ya kichanga ambayo mara nyingi ina rangi ya light brown. ardhi ya kichanga haiweki madimbwi ya maji wakati wa mvua kubwa (note kama ardhi inaweka maji mengi juu au madimbwi matikiti yanaoza). kwa mavuno mazuri anza kupiga dawa wiki 3 baada ya kupanda, anza kupiga mocron inasaidia kuua wadudu piga after every 2 weeks. ( kuna dawa za aina nyingi za wadudu, fungus pamoja na booster ya kusaidia kukuza matunda haraka). matkitimaji yanachukua mda wa miezi 2 na nusu mpaka mi3 kuanza kuvuna. soko liko kubwa, juhudi kutafuta. dummies
 
Acha habari za naskia...fanya utafiti.

Kwa kuanzia nakushauri upite pale sokoni kariakoo, lile linaitwa soko la zamani au soko la nazi, tafuta mfanyabiashara ya viungo kisha muulize manga inauzwaje kwa kilo(bei ya reja reja) na yeye yupo tayari kununua kwa kiasi gani kutoka kwa mkulima(ambaye ni wewe), mueleze ukweli tu kuwa unafanya utafiti na kwamba unakusudia kulima manga. Hapo utapata picha halisi ya mambo yalivyo na si kuishi kwa naskia, naskia.

Nimewahi kupata mawazo kama yako ya kulima manga, nikatafiti wapi inastawi...niliambiwa pahala fulani ndani huko mahenge, usafiri ni wa treni ya tazara vinginevyo uwe na four wheel drive kama land rover defender au landcruiser mkonga, nilichogundua ni kuwa si jambo jepesi sana kulima spices kama manga, hiliki na mdalasini, ni changamoto kama ilivyo changamoto yetu ya kila siku ya kuamka asubuhi kwenda kazini mpaka saa 11 jioni.

Wakuu! Heri ya 2013 !
Baada ya kuona maongezi haya ya kilimo cha pilipili manga, nikaamua kufanya utafiti alau kidogo kama ulivyoshauri.
Nimepita kkoo sokoni leo nikaongea na jamaa anaeuza viungo. Nimemuambia tu kuwa ninae jamaa yangu huko Turiani Morogoro (maana najua huko wanalima pilipili manga) amenipigia simu akaniomba nimsaidie kujua bei ya kuuza pilipili manga hapa sokoni kkoo kwa sasa. Jamaa muuza spices akauliza kwani ana gunia ngapi? nikamwambia sina uhakika sana ila hakosi kama 5 hivi. Jamaa akasema nimwambie huyo ndugu yangu wa Turiani kuwa bei ya Manga kwa sasa imeshuka maana wananunua kwa sh 7,000/- kwa kilo moja. Eh Eh ! nikashtuka kimya kimya maana kwa mimi 7,000/- kwa kilo ni bei kubwa japo sijui gharama za kuzalisha! Nikamuuliza mbona bei imeshuka kwani nyie kwa reja reja mnauzaje? Akajibu "Kwa sasa tunauza Elfu Kumi kwa kilo"

Nikamwuliza, je kama jamaa yangu akija na huo mzigo atauza haraka au itabidi asubirie sana wanunuzi? "We mwambie tu alete wanunuzi wapo wengi hapa sokoni". Nikamwambia asante, nitamjulisha alete.
Toka hapo nikasogea mbele zaidi kwa muuzaji spices mwingine. Nikamwuliza ataniuzia bei gani pilipili mtama kwa kilo moja. Akajibu kilo moja ni sh elfu kumi na mia tano. kama nachukua kilo zaidi ya tatu atanifanyia elfu kumi kamili. nikamwambia bei yako kubwa sana mzee ngoja nizunguke na kwa wengine.

Wakuu hiyo ndiyo habari kuhusu bei ya pilipili Manga sokoni Kkoo. Ni busara kufanya utafiti zaidi huko wanakolima hili zao ili kuona uwezekano wa kushiriki kilimo hiki. Bei inaonekana nzuri lakini pengine hadi upate gunia moja au mbili shughuli yake ni pevu, na ndiyo maana wakulima wa hili zao sio wengi.

Nitaenda Turiani hivi karibuni na nikirudi nitaweka story yote hapa jamvini.
 
mkuu ... please awaiting for your feedback anxiously
 
Ni shamba au eneo la ukubwa gani inabidi uwe nalo kuzalisha gunia 100 za maharage?
 
Ukiona kitu kinauzwa bei ya Juu ujue kunashughuli pevu kwenye kutengeneza, Nakumbuka Huku Arusha kuna Aina fulani ya Mbegu za maua ambazo hulimwa natheni unauz zile mbegu zake make zina kazi huko ULAYA, Kilo Moja ya Hayo maua ya Megu ni 300,000, na yapo ambayo kilo ni 50,000 sasa shughuli yake si ya kitoto kabisa, kupata mbegu za kutosha ni kazi ya ukweli, n unaweza lima shamba ima ukaambulia kilo mbili tu, au hata kilo Moja
 
Matikiti, mananasi yote matatizo matupu...vijana wa hapo dar walidanganyana sana miaka kadhaa iliyopita kwamba ni fast money making ways. wakavamia mashamba kiwangwa, bunju na chanika kulima mananasi na matikiti, wengi waliambulia hasara na sasa wametambua kwanini babu zao walilima na wamekufa masikini..kilimo si kazi ya watu masikini.
Kilimo si jazi ya maskini, ila mkulima ndio masjini
 
Back
Top Bottom