Lima matikiti maji km eneo lako lina upatikanaji wa maji wa uhakika kwa ajili ya umwagiliaji.
ngwara inatambaa sana hivyo inahitaji eneo kubwa. Alaf pod zake haizai zaidi ya punje tatu. Ni kweli ina bei nzuri lakini uwe na eneo kubwa
Inastawi eneo gani?
Vipi kulima pilipili manga? Nasikia gunia moja unakula 600,000
Uncle, unaweza ukachanganua kidogo kwenye hili la matikiti maji? Au kama kuna thread humu ilishawahi kuzungumzia ntashukuru kama uki post hapa.
matikiti, mananasi yote matatizo matupu...vijana wa hapo dar walidanganyana sana miaka kadhaa iliyopita kwamba ni fast money making ways. wakavamia mashamba kiwangwa, bunju na chanika kulima mananasi na matikiti, wengi waliambulia hasara na sasa wametambua kwanini babu zao walilima na wamekufa masikini..kilimo si kazi ya watu masikini.
Acha habari za naskia...fanya utafiti.
Kwa kuanzia nakushauri upite pale sokoni kariakoo, lile linaitwa soko la zamani au soko la nazi, tafuta mfanyabiashara ya viungo kisha muulize manga inauzwaje kwa kilo(bei ya reja reja) na yeye yupo tayari kununua kwa kiasi gani kutoka kwa mkulima(ambaye ni wewe), mueleze ukweli tu kuwa unafanya utafiti na kwamba unakusudia kulima manga. Hapo utapata picha halisi ya mambo yalivyo na si kuishi kwa naskia, naskia.
Nimewahi kupata mawazo kama yako ya kulima manga, nikatafiti wapi inastawi...niliambiwa pahala fulani ndani huko mahenge, usafiri ni wa treni ya tazara vinginevyo uwe na four wheel drive kama land rover defender au landcruiser mkonga, nilichogundua ni kuwa si jambo jepesi sana kulima spices kama manga, hiliki na mdalasini, ni changamoto kama ilivyo changamoto yetu ya kila siku ya kuamka asubuhi kwenda kazini mpaka saa 11 jioni.
Wakuu! Heri ya 2013 !
Baada ya kuona maongezi haya ya kilimo cha pilipili manga, nikaamua kufanya utafiti alau kidogo kama ulivyoshauri.
Nimepita kkoo sokoni leo nikaongea na jamaa anaeuza viungo. Nimemuambia tu kuwa ninae jamaa yangu huko Turiani Morogoro (maana najua huko wanalima pilipili manga) amenipigia simu akaniomba nimsaidie kujua bei ya kuuza pilipili manga hapa sokoni kkoo kwa sasa. Jamaa muuza spices akauliza kwani ana gunia ngapi? nikamwambia sina uhakika sana ila hakosi kama 5 hivi. Jamaa akasema nimwambie huyo ndugu yangu wa Turiani kuwa bei ya Manga kwa sasa imeshuka maana wananunua kwa sh 7,000/- kwa kilo moja. Eh Eh ! nikashtuka kimya kimya maana kwa mimi 7,000/- kwa kilo ni bei kubwa japo sijui gharama za kuzalisha! Nikamuuliza mbona bei imeshuka kwani nyie kwa reja reja mnauzaje? Akajibu "Kwa sasa tunauza Elfu Kumi kwa kilo"
Nikamwuliza, je kama jamaa yangu akija na huo mzigo atauza haraka au itabidi asubirie sana wanunuzi? "We mwambie tu alete wanunuzi wapo wengi hapa sokoni". Nikamwambia asante, nitamjulisha alete.
Toka hapo nikasogea mbele zaidi kwa muuzaji spices mwingine. Nikamwuliza ataniuzia bei gani pilipili mtama kwa kilo moja. Akajibu kilo moja ni sh elfu kumi na mia tano. kama nachukua kilo zaidi ya tatu atanifanyia elfu kumi kamili. nikamwambia bei yako kubwa sana mzee ngoja nizunguke na kwa wengine.
Wakuu hiyo ndiyo habari kuhusu bei ya pilipili Manga sokoni Kkoo. Ni busara kufanya utafiti zaidi huko wanakolima hili zao ili kuona uwezekano wa kushiriki kilimo hiki. Bei inaonekana nzuri lakini pengine hadi upate gunia moja au mbili shughuli yake ni pevu, na ndiyo maana wakulima wa hili zao sio wengi.
Nitaenda Turiani hivi karibuni na nikirudi nitaweka story yote hapa jamvini.

Kilimo si jazi ya maskini, ila mkulima ndio masjiniMatikiti, mananasi yote matatizo matupu...vijana wa hapo dar walidanganyana sana miaka kadhaa iliyopita kwamba ni fast money making ways. wakavamia mashamba kiwangwa, bunju na chanika kulima mananasi na matikiti, wengi waliambulia hasara na sasa wametambua kwanini babu zao walilima na wamekufa masikini..kilimo si kazi ya watu masikini.