Nimesoma komenti tangu mwanzo hadi hapa.. Ila bado sijapata content ya kujitosheleza.. Hasa kwa sisi wageni ambao tunashawishika kulima zao la nyanya..
Kilimo cha nyanya , ni project kama project zingine tuu.. Hivyo inahitaji mambo kadha wa kadha wa kuyajua. Mfano, ujue gharama ya from beginning to end, gharama ya kuvuna, na faida zake; hii itategemea na ukubwa wa shamba, kama ni kwa robo eka, nusu au ekali nzima..
Sasa inaonyesha is like wengi wetu tunaingia bila kujua mchanganuo... Changamoto nk.
Story zimekuwa nyingi, kila utaalamu adi mtu unashindwa kujua ufanyeje..
It seems like humu kuna wakweli na matango pori..
Mbaya zaidi sasaivi sisi wanadamu hasa watanzania tunapokea kila kitu kutoka nje huko. Hao wa nje wanatuletea kila kitu skuiz chotara na feki za muda mfupi ili tuendelee kuwategemea..
Yaani imefikia hadi sasa ivi hatuwezi tena kutengeneza mbolea ya mboji ya asili, tunataka shortcut.. Hii imetulemaza sana.
Kuna mzee mmoja mahali flan ana shamba la ekali kama moja, analima mahindi.. Analima kilimo cha mkono tuu, anaweka mboji, kwenye ukuzaji anatumia ya kuku na ng'ombe, kila wakati anatembelea shamba, anafanya parizi mda wote, shamba liko saaafii mda wote, kila wakati anaweka mbolea hizo pale anapoona inabidi... Yaani mahindi yake yananyanyuka hatareee yanabeba baraaaa...
Lakini sisi vijana skuiz tumekuwa brain washed na hao washenzi wa nje.. Wanatengeneza strategic programs, wana zi publish kwa nguvu zoooteee.. Sisi tuna vitu vingi vya asili ambavyo ukiwa creative unaweza ukalima bila ya kutumia hayo madawa yao kwa sana, na ukafanikiwa..
Nimefanya studies kadhaa, believe me o not,, hayo madawa na mambolea yao, ndio in returns yanaleta madudu kibao.. So, itafika mahali kuna siku TUTALETEWA HADI UDONGO WA KUUZWA AMBAO UTAKUWA UNAFAA KWA KILIMO.. Usipo tumia akili utasema haiwezekani.. Nikwambie sasa.. Wataleta madawa ambayo watakuambia uchanganye udongo wako na hayo madawa kabla ya kuweka mbolea, na utatii, then watakuambia nunua pumba spesho kutoka wapi sijui, uziweke juu yake kabla ya mbolea, na utatii.. Hawa jamaa wana propaganda ambazo zina tu brain wash akili zetuu zoooteee tuna wawaza wao tuu..
Inafikia mahali kijana anapata ka milioni kake kamoja,, anatamani kulima nyanya, anapata ushauri mbaya wa kwamba ela haitoshi.. Wakati iyo milioni moja analima vizuri tuu hata ekali mbili, kama akichanganya utundu wetu wa asili tuliokuwa tukiutumia kwa kuufanya modify kidogo kuendana na mazingira plus ata kumwagilia kwa mkono, na akatoboa.
Lakini leo,,,, tunakuwa propagate kila konaaaaaaa tutumie ela nyingiii kulima. Ili wachache walime.. Shame on us..
Nimechukia sanaaaaa