Kilimo cha parachichi ni njia rahisi ya kuufikia utajiri mkubwa

Kilimo cha parachichi ni njia rahisi ya kuufikia utajiri mkubwa

Asante sana mkuu TREE OF LIFE FOUNDATION kwa kushirikisha mawaza haya...nimenunua ardhi Kilindi Tanga na nimesafisha kwa sehemu...ili kuifikia ndoto ya kuwa mkulima wa kati na hatimaye mkubwa...bado naendelea na kautafiti mdogo.... hizi Parachichi za Hass kweli nasikia zina soko ila temperature ya pale kilindi naihofia ina-range between 17-31 degree-Centigrade
Mkuu TAJIRI MKUU WA MATAJIRI uzoefu wako wa Newala ukoje bro..
Kwanini HASS, kwa sababu inakaa muda mrefu rafuni(Shelf life) hadi mwezi mzima bila kuharibika na hapa ni pale tu ikitunzwa kwenye Good Condition(5°C).

Parachichi inapandwa kwenye eneo lenye Altitude 0-2000's asl ila the best for Hass variety tunayoilima kwa wingi nyanda za juu kusini ni Mita 1800-2000 asl na hii ni kwa ajili ya uwekaji mzuri wa mafuta. So Kilindi huwezi Lima Parachichi kibiashara mkuu. Napajua huko pana joto sana.
 
tatizo soko mkuu....niko morogoro wilaya ya mvomero.. nina shamba la parachichi.. kwa huku shambani tunauza sh. 50 kwa parachichi moja

kama huto jali kaka nipe connection ya soko nilete mzigo wangu mkuu

nitashukuru sana

0655 944268
Mvimero sehemu gani na umesimama variety gani mkuu. Variety hass ndio nzuri kwani ina mafuta mengi, ganda gumu na lenye vinundu, lina dumu muda mrefu bila kuharibika na lina soko la uhakika ndani na nje ya nchi.
 
Katika vitu ambavyo amuongelei ni critical managerial practices to reach maximum production nimetembea na kuwaonea huruma baadhi ya wakulima uko njombe na mbeya Miti ya parachichi unakuta umedumaa zaidi ya miaka minne hadi mitano hakuna dalili hata ya kuweka Maua, Miti kuendelea kukauka Kwa taratibu, huduma ya umwagiliaji kuwa hafifu sana maana parachichi inaitaji maji ya kutosha iweze kutoa mavuno Kwa misimu miwili angalau, changamoto ya kupukutika Kwa Maua na mkulima kuambulia trey 1 tu kwenye mti mzima . Jaribuni kuonyesha solution za hizo challenge Ili mtu ambaye sio expert on that field ajue the way forward before engage in avocado industry.Asante
Ni sahihi, Parachichi ni moja wapo la "high value crop" lina hitaji mtaji mkubwa kuliko manage hususan kwenye Maji, ratiba nzuri ya mbolea na upigaji sahihi wa viuatilifu.
Ni kweli kabla ya kuingia kwenye hiki kilimo ni lazima ujiande kiuchumi kwani ili kwa miaka 2-3 iweze kuzaa inahitaji close management with high amkunt of money i.e lazima uwe na nguvu ya kiuchumi. Mkuu, ukilihudumia vizuri ni uchumi na utajiri. Mi nipo Rungwe mkuu naona kazi inavyofanyika na uchumi tulionao.
 
Write your reply...Nimezunguka sana kutafuta utajiri nikaona kilimo kinaweza nifanya kuwa tajiri, huwa natamani sana kupanda hata zaidi ya hekari 10 lakini changamoto kubwa inakuwa ni jinsi gani ya kupata miche ya kisasa. Huku kwetu mkoa wa Rukwa ni kama upatikanaji wa miche ni changamoto sana, Kama ingekuwa inapatikana ningefanya juhudi nitenge hata hekar 5
Rukwa sehemu gani? Kabla hujaagiza miche sema ili nikushauri bro. Najua Rukwa na Katavi yote pia nipo kwenye Kilimo cha Parachichi kwa muda mrefu sasa.
 
From morogoro Ila nimekuja kuwekeza njombe.nimelima parachichi hass na adi sasa natimiza miezi 6 tangu nipande hii miti kalibuni wazee na vijana wenzanguView attachment 2642897
Hii miche umeitoa wapi? Mbona kama siioni hass hapo. Hass ni lazima majani yawe kijani tii, yawe membamba na yamechangia na hayo mapya yanakuwa kama yana mafuta.

Hapa ni muhimu sana kwenye kuchagua na kuwa na uhakika na miche kwani unaweza jua ni hass kumbe ni locla variety. Miche mingi ya Morogoro mnaambowa Hass but sio hass. Niliona pale kwenye Bustani za mbegu za miti Morogoro na hata jamaa yangu Emanuel aliniletea toka Moro. Hii kama sio Hass kwa nionavyo bro.
 
Wakati nanunua pori kule Tukuyu, enzi hizo nikiwa mwajiriwa kinda kabisa PPF Head Quarters watu walinicheka sana.

Nilipowaambia ndoto yangu ni kulima parachichi walinikebehi kwa maneno mengi ya shombo. Wengine wakaniambia bora niwe dalali soko la Mabibo kuliko niwe mkulima.

Maneno yao ya kunikatisha tamaa, yakanichoma, nikasema kwenye kupigwa vita ndio kuna ushindi. Nikaacha kuwaeleza mambo yangu.

Basi kila ijumaa jioni naondokea kazì, nawahi hakuna kulala na wakati mwingine gari za IT na za magazeti, asubuhi niko shambani Tukuyu.

Leo kila mtu anatamani awe kama mimi. Sijawa mchoyo, nimekuwa mwonyesha njia kwa yeyote anayenifuata.

Kilimo cha alizeti Mbeya na Njombe, kilimo cha mahindi, kilimo cha mpunga Kamsamba, ufugaji ng'ombe wa maziwa nk vinanifanya nitambe.

Sasa rasmi nimeingia kwenye kilimo cha soya beans kwa ajili ya exportation. Hii nchi kuna fursa sana lakini vijana wanaziona miyeyusho.
Natamani ungeandika na kitabu chenye huo ushuhuda halisi wa mafanikio. Hongera sana mkuu.
 
Kwanini HASS, kwa sababu inakaa muda mrefu rafuni(Shelf life) hadi mwezi mzima bila kuharibika na hapa ni pale tu ikitunzwa kwenye Good Condition(5°C).

Parachichi inapandwa kwenye eneo lenye Altitude 0-2000's asl ila the best for Hass variety tunayoilima kwa wingi nyanda za juu kusini ni Mita 1800-2000 asl na hii ni kwa ajili ya uwekaji mzuri wa mafuta. So Kilindi huwezi Lima Parachichi kibiashara mkuu. Napajua huko pana joto sana.
Mkuu, vipi kwa Kakonko mkoani Kigoma?
 
Back
Top Bottom