kasanzu elias
New Member
- Feb 20, 2013
- 2
- 1
Kutokana na kutokuwa na mvua za uhakika na za wakati kwa baadhi ya maeneo hapa inchi imepelekea maisha ya wananchi wengi hasa vijijini kuwa magumu kwa sababu tegemeo lao kubwa ni kilimo cha mazao ya chakula au biashara, ambacho pia ndio tegemeo lao la kukomboa familia zao kiuchumi, elimu, Afya na ujenzi wa makazi bora.
Kwa upande wangu nimeona fursa ya wanachi hasa kwa mikoa ya Tabora, Shinyanga na Simiyu, kuweza kuchochea ushiriki wao kwenye sekta ya kilimo cha umwagiliaji kwasababu maeneo mengi ya mikoa hii ina miamba ya maji ambayo haipo mbali sana kutoka juu, na watu walio wengi wamejichimbia vijisima vya mita 1 hadi 5 na wanaweza kujipatia maji kipindi chote cha mwaka
Namna ya kulitekeleza hili kwa upande wangu kama kupitia stori hii itaweza kuwavutia,
Kwanza kabisa ni kutafuta maeneo katika mikoa tajwa hapo juu ambayo nitaweza 1.kujimba visima vya kuanzia mita 25 hadi 30
2. Ununuzi wa pampu za maji za pawa tila zilizoboreshwa
3. Ushirikishwaji wa wanachi watakao kuwa wanazunguka visima kuweza kushiriki kilimo cha umwagiliaji kwa kuchangia kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya uendeshaji wa visima, ununuzi wa mipira, ununuzi wa mafuta ya kuvuta na kusukuma maji, Kulipa vijana watao kuwa wanahusika katika chaini hii kama mafundi, walinzi
Na kwa wananchi ambao watakuwa hawana uwezo wa kutoa kiasi cha pesa nitawasaidia kwa kuingia nao ubia, yaani wao wawekeze nguvu ya kuanda shamba na mbegu na mengine, kisha kwa upande wangu niwekeze nguvu ya kupeleka maji kwenye mashamba yao.
Ninaamini kupitia wazo hili litagusa wananchi wa vijijini moja kwa moja na pia litachochea watu wengine kuona fursa hii yenye uhakika kwa baadhi ya mikoa hapa nchi kwetu

Upvote
1