Kilimo cha uyoga

Wernery G Kapinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Posts
376
Reaction score
127
Habari wadau wote wa JF. Binafsi Niko kwenye maandalizi ya KILIMO Cha UYOGA. Hivyo nataka nianze kidogo kwa ajili ya familia. Nimesoma na kuangalia kwa umakini kabisa, Nataka nianze kwanza kwa ajili ya familia.

Changamoto kwangu ni upatikanaji wa mbegu. Tafadhali mwenye ushauri huu ya hili maana nimeshapigwa 20,000/= kwa kuchukua namba mtandaoni na kusubiria kutumiwa. Tafadhali mnisaidie kwenye uhakika ambako naweza agiza mbegu za UYOGA na nikatumiwa.
 
Nipo kwenye group la wakulima wa kisasa ngoja nikuulizie supplier.

Kwanza upo mkoa gani nijuwe? Maana kwa Morogoro SUA ndio rahisi.
 
Arusha kuna mama mmoja ni mtaalamu wa muda mrefu na anaaminika sana, hufadhiliwa kutoa mafunzo...
Anapatikana maeneo ya Tengeru...jina maarufu mama Kaaya
 
Ulipata ndugu? Na kama umedhamilia,kwa nini usiangalie wapi pana uhitaji,uchukue mzigo wa kutosha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…