Vanilla si kama figisu za kware au matikitimaji Root. Vanilla inauzwa katika international markets. Hata hapa Tanzania kuna viwanda vya chai vinanunua vanilla kuchanganya kwenye chai. Watengeneza kahawa (grade 1), Icecream na viburudisho mbalimbali wanahitaji vanilla. Shida ya vanilla kwa bukoba inaathiriwa sana na ukame/mabadiliko ya tabia nchi kwani vanilla inahitaji mvua nyingi sana. Pia uwekezaji uwe tayari kuvumilia miaka 3. Na mdau mmoja kasema hakuna natural pollination katika vanilla, lazima uwe na vibarua wa kutosha tena waliofundishwa kufanya uchavushaji wa maua ndani ya siku 2.
Nilisikia morogoro na mbeya wanalima ingawa sina taarifa kamili. Nafahamu vyama viwili vya wakulima wa vanilla bukoba; moja Kamachumu vanilla farmers association kilichiopo Kamachumu Wilaya ya Muleba na Maruku farmers assocoaition sijui iko wapi.