Kilimo cha Vanilla nchini Tanzania

Biashara ya Vanilla inalipa sana ila kwa Tz naona bado sana
Nimenunua na kuuza sana ila ilikuwa inatoka Madagascar na unatuma hela mzigo unapokea Airport bila longolongo na uaminifu mkubwa
Hii biashara kuna nchi wanalima na wanalinda kwa bunduki kwani ni ghali mno
 
Mkuu,
Msije mkaingia kichwa kichwa,mambo sio marahisi hivyo, Mosi Taarifa VANILLA INTERNATIONAL LIMITED kwa kiasi kikubwa sio kweli, Marando ya vanilla bei yake sio 20,000= bei yake ina range kati ya 3000 mpaka 5000

Bei ya vanilla duniani mara nyingi inapanda na kushuka na hii inategemea hali ya soko la Madagascar ambao ni waalishaji wakubwa duniani...kwahiyo mwaka huu inawea ikawa kubwa mwaka ujao ikawa ndogo, tangu nianze kulima vanilla sijawahi na wala sijui kama ntakaa niue kilo moja beans kwaaidi ya TSH Milioni kama wanavyotangaa

Ushauri wangu...kilimo cha vanilla sio kibaya ila kabla ya kuingia tambua

1- Ni labor intensive , uchavushaji wa vanilla unatumia mikono

2-WeZi; kwa maeneo hususan ya kagera na baadhi ya maeneo ya kilimanjaro kipindi cha mavuno kunakuwa na wii mkubwa saana

3- Jua soko lko au soko la hao wanaukulimia, kwa kiasi kikubwa wakulima wengi wanaingia hasara kutokana na kutokujua soko lake, mtu anaenda kulima akishakaribia kuvuna ndio anarudi mezani kaunza kufirikia atamuuzia nani...hapa nashauri kabla hujaenda sokoni plz anza kutafuta soko kwanza ikiwezekana ingia namnunuzi mkataba

4...Jifunze utambue ABC za vanilla, hii itakusaidia kuepusha kudanganjwa

5- Nashaurii ukilima vanilla plz panda kwenye shamba lako mwenyewe, mche wa vanilla unaweza dumu mpaka miaka 40 ukiangaliwa na kuhudiumiwa vizuri

Hitimisho

Mimi nalima vanila kwa mkataba ( contract farming), mapato yake sio kama yanavyotangazwa na hawa wajasiriamali. ninaliama na kampuni ya .....Natural Extracts Industries Ltd...hawa ndio wanaonunua, na wananipa huduma za ugani

Muwe na kilimo chema
 
MOTIVESHENI SUPIKAZ 😅😅

Vanilla uchavushaji inampasa binadamu mkulima kukesha mashambani akihamisha pollens kwenye maua from male to female parts,

Pia huwezi kulima kwenye open space kazi na kuwe na kivuli n.k
Ni changamoto na huvunwa inapokuwa inakauka kuelekea kuharibika, ili iwe ya kiwango cha quality nzuri.

Wengi hapo kwenye uchavushaji ni tatizo pia hali ya hewa, usipochavusha hakuna mavuno ya vanilla.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Nilimsikia baba levo akipiga porojo kuhusu hio vannila ila kwa spana nilizopigwa mashambani hamna jinsi utanishauri nilime!
Watu walime mie ntanunua tu kisha niuze katika soko langu nalojua mimi!
 

Unaielewa vizuri sana hili zao
Bora umetoa darasa la pollination
 
Nilimsikia baba levo akipiga porojo kuhusu hio vannila ila kwa spana nilizopigwa mashambani hamna jinsi utanishauri nilime!
Watu walime mie ntanunua tu kisha niuze katika soko langu nalojua mimi!
Wezi hao, swagga nyingi, hawaongelei ugumu wa kuchavusha, iwe jua iwe mvua, hizo siku za kupata mimba maua usipochavusha basi, usubirie msimu ujao,
Na bei wanazokuja nazo ni uongo mtupu.
Wanaandika bei ya vanilla iliyokuwa graded highest quality huko ulaya na siyo shambani Matombo huko.

Hawana tofauti na Namaingo, Kijani kibichi n.k

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Wale wa kupenda hesabu za kwenye makaratasi wataingia 18% na watabutuliwa kama kawaida
 

Machame, Kilimanjaro zinalimwa kwenye open space.
 
Wale wa kupenda hesabu za kwenye makaratasi wataingia 18% na watabutuliwa kama kawaida
😅 Kilimo cha WhatsApp, ngoja wauziwe marando ya vanilla, wakifikiria hicho sawa na kilimo cha tembele Kibaha au manumbu Gairo.

Tusubirie mirejesho ya wakurupukaji!

Everyday is Saturday................................😎
 
Huyu jamaa wa Vanila international ni tapeli though ni mzur katika marketing. Kabla ya hapo alikuwa na kampuni anaiita greenhouseinteenational.ltd.

Sasa hivi kaja na mbinu nyingine. Jamaa ni opportunist mzuri sana.
 
Mkoa gani vanilla inastawi
 
Pesa haziji kirahisj hivyo,yaani umeweka mbupu juu tu uletewe maarifa.
Kaka punguza hasira, kama una taarifa njoo nambie mahitaji yako nikimudu utanipatia elimu, kama sitoweza si basi kaka, hakuna sababu ya hasira na povu jiiiingi bila sababu, kwa umri wangu nafahamu hakuna elimu bure.
Punguza hasira.
 
Umeeleza vyema sana mtaalamu , lengo langu lilikuwa watu kujua , hii naona ni aina mpya ya upigaji tuu hakuna msaada wowote kwa mkulima
 
Huyu jamaa wa Vanila international ni tapeli though ni mzur katika marketing. Kabla ya hapo alikuwa na kampuni anaiita greenhouseinteenational.ltd.

Sasa hivi kaja na mbinu nyingine. Jamaa ni opportunist mzuri sana. View attachment 1758946
Hiyo green house international iliishia wapi mzee niliisikia sana pia , walikuwa wanasema Wana soko kubwa Comoro
 
Mkuu samahani naomba mawasiliano yako ,nahitaji kujua zaidi maana huku niliko watu wanafuatilia kiukaribu hii issue ya vanilla kwa hiyo nakuomba unipe namba yako au Kama ikiwezekana nibip tu namba hii hapa 0673034335, Natanguliza shukrani Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…