Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa mda huu ni sahihi kulima ukizingatia mwaka huu mvua zinazingua kweli na mwezi April katikati inategemewa mvua zitakata..ushauri tafadhali maana nina mahali pamebaki na sijamaliza kupanda.Dodoma ni sehemu nzuri pia ya kulima ufuta na unastawi vizuri changamka tafuta shamba ulimi
Pia nadhani muda si sahihi jaribu kujipanga msinu ujao G3T,kilimo kinahitaji maandalizi makubwa kabla ya kupanda....kuliko inavyodhaniwa ushauri wangu nendaa maeneo yenye mvua za kutosha lindi,sumbawanga,manyara
@MrGenius vipi kuhusu vifaa vya kupandia kwa Tanzania vipo ?
Mkuu sijajua kama vipo au la! Kwakua sijawahi kuviona, mana wakulima wengi hutumia njia ya mkono tu! Ingawaje baadhi ya wakulima wameongezea ubunifu kwa kutia zile mbegu wanazotaka kuapanda kwenye vichupa vya maji kama vile vya uhai na kisha kutoboa kitundu kidogo sana kwenye kizobo kiasi cha kuruhusu kiasi cha mbegu tano au saba tu kupenya wanapobinya kwenye shimo!!

Nimefuatilia uzi huu kwa makini, na kuona mengi sana yameshazungumzwa kwa kua na mimi kilimo ndio taaluma yangu nimeona niwasaidie wakulima humu kwa kujazia machache kwa kua meng yalisha semwa mi nitajikita kidogo hapo kwenye upandaji kwanza niwaambie tu kwa wale mliopanda mbegu ya lindi 02, hiyo ndio mbegu 'the best choice' kwa sasa ambayo tunamshauri mkulima apande. Mbegu hii iliyofanyiwa utafiti na kituo cha utafiti cha kilimo naliendele na kisha kua 'released' mwaka 2002 inasifa zifuatazo
-ni mbegu nyeupe zaid kuliko naliendele 92 na ziada 94
-inamafuta meng kias cha 55%
-Haiendi juu sn kwa kimo
-inamatawi kuanzia 5-7
-pods zake inch moja had mbili
-inakomaa mapema na kua tayar kuvunwa baada siku 100-110 (hivyo ni kama baada ya miez mitatu
)
-Huvumilia ugonjwa wa madoa ya majan (leaf spot)
Tukija kwenye upandaji sasa
The commonly methods used
1)Drilling (kuchmba kjmferej)
2)Dibbling (kupga mashimo moja moja)
3)Broadcasting (kusambaza kwa kumwaga shamban)
Najua wengi hum ndani mshapanda ufuta na njia hizi hua mnazitumia sana kwa hiyo mnafaham, lakini katika zote hizo hapo juu nilizo zitaja hii njia ya kusambaza hua hatuishauri sababu haijakaa kitaalamu kwanza ni vigumu kukadiria spacing sabab mbegu na miche itakayotoka itakua imezagaa na hivyo hata kukadiria mavuno ni vigumu (yield estimation). The sowing depth of simsim is advised to be 2cm deep then 5-10 seeds are placed.
Apacing is 50cm mstar had mstar this is for dwarf varieties and
75cm mstar had mstar for tall varieties.
And 10cm toka shina moja la ufuta kwenda lingne!!
*mbegu hii ya lindi 02 is among dwarf varietis hivyo spacing yake yapasa iwe 50cm mstar had mstar wengne wanawekaga 60cm hata 65 kutegemeana na rutuba iliyopo kwenye udongo!
La mwisho kwa kuongezea mbegu za ufuta ni ndogo sana kwa maana ya punje zenyewe hivyo wakati mwingne ku-control usimwage nyingi kwenye shimo au kamfereji wakati wa kupanda tunashauri ni bora ukazichanganya na mchanga mf:-ukitumia kasufuria kupimia ufuta (wakati unataka uchanganye na mchanga) basi utaweka kisufuria hiko hiko cha mchanga mara nane yaani katika ratio ya 1:8
Makadirio ya mavuno ya ufuta kwa mbegu ya lindi 02 tunategemea hadi 1500kg per ha (tan 1.5) na kwa ekari moja makadirio kuanzia 500kg-700kg under favourable conditions and good menagement.
Na kias cha mbegu unachotakiwa kupanda kwa ekari moja (seed rate) ni kuanzia 1kg-1.5kg
Najua pana wataalam wenzangu hum wengi tu na wakulima wazoef pia kama nyinyi hivyo mtajazia au kusahihisha karibuni mjadala uendelee!!
Hiyo mbegu ya Lindi 02 ntaipata wapi? maana ufuta imekuwa issue kupata mbegu.
Mkuu sijajua kama vipo au la! Kwakua sijawahi kuviona, mana wakulima wengi hutumia njia ya mkono tu! Ingawaje baadhi ya wakulima wameongezea ubunifu kwa kutia zile mbegu wanazotaka kuapanda kwenye vichupa vya maji kama vile vya uhai na kisha kutoboa kitundu kidogo sana kwenye kizobo kiasi cha kuruhusu kiasi cha mbegu tano au saba tu kupenya wanapobinya kwenye shimo!!
Mkuu subiri miezi ya october hadi december ndo unazipata kwa mawakala wa mbegu. Nimeitafuta juzi kati ikawa imeisha kila sehem.
Ahsante mkuu nawe n mkulima Wa ufuta?
Mi nataka kufaham kwa shina moja libabeba wastani wa pods ngapi wakuu.Ndio mkuu nami nalima. Karibu kwenye ujasiriamali
mi nataka kufaham kwa shina moja libabeba wastani wa pods ngapi wakuu