Katika jamii yeyote ili watu waweze kuwa na uhakika wa kuishi na kufanya shughuli zao za kila siku basi lazima kuwepo na uhakika wa usalama wa chakula,kwani chakula ni hitaji la lazima katika maisha ya binadamu. Uhakika wa upatikanaji wa chakula katika eneo fulani unachangiwa na uwepo wa sera madhubuti zinazohakikisha kuwepo kwa ustawi wa kilimo na kuhakikisha sera zinahamasisha kilimo ili kuhamasisha watu kujishughulisha na shughuli za kilimo kwa maslahi ya taifa.
Nchini Tanzania kilimo ni uti wa mgongo kwa wananchi walio wengi,takribani asilimia Zaidi ya 70 ya watanzania hujishugulisha na shuguli za kilimo.Sekta ya kilimo huchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa.Kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya dunia kuhakikisha kunakua na usalama wa chakula duniani, Serikali ya Tanzania kupitia sekta ya kilimo na kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa program na agenda mbalimbali za kuendeleza sekta ya kilimo ili kuweka msukumo kwenye maendeleo ya uchumi kwa kuzingatia vipaumbele vya maendeleo na dira ya Taifa ya mwaka 2025 ili kuleta mageuzi na kuongeza uzalishaji na tija ili kilimo kiwe cha biashara Zaidi ili kuongeza pato la wakulima na taifa kwa ujumla. Serikali imeandaa agenda na mikakati mbalimbali kama,
Kuweka mazingira wezeshi ya kuendeleza sekta ya kilimo, imeandaa Mkakati wa kutoa ruzuku ya mbolea ili kushuka kwa bei ya mbolea, na serikali kupanga bei elekezi ya mbolea na kusajili wauzaji wa mboleaa ili kuuza mbolea kwa bei elekezi ya serikali kuepuka kupandishwa kwa bei ya mbolea kiholela.
Pia serikali imeanzisha mchakato wa kuanzisha vitalu na viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na usindikaji wa mazao ili kuongeza uzalishaji na kulinda maslahi ya wakulima ili kuongeza ustawi katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo.
Vilevile wataalamu wa kilimo kuzalisha mbegu bora za mazao ili wakulima nchini waongeze tija na uzalishaji, pamoja na kuanzisha mashamba ya pamoja (block farms) katika mikoa tofauti ili kusaidia ushiriki wa vijana katika shughuli za kilimo.
Licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuendeleza kilimo nchini,lakini bado wakulima wengi hawajajikita katika kilimo kibiashara kutokana na changamoto mbalimbali zinazosababisha wakulima wengi kushindwa kupata matokeo chanya,changamoto hizo kama,
Kupanda kwa gharama za uzalishaji, wengi hushindwa kujihusisha na shughuli za kilimo kwa kiwango kikubwa au kushindwa kufikia lengo la kilimo biashara kutokana na upandaji wa gharama za uzalishaji ikiwemo bei kubwa ya mbegu ,mbolea, na viuatilifu pamoja na nyenzo nyingine muhimu ambazo hutumika katika shughuli za kilimo cha mazao.
Bei zimekua kubwa na kusababisha mtu wa kipato cha chini kushindwa kumudu gharama, kwani ili uweze kupata matokeo bora basi unahitaji mbegu bora kulingana na ardhi ya eneo husika, mbolea ya kutosha itakayosaidia ustawishaji wa mmea vizuri ili kuleta matokeo mazuri pamoja na madawa kwa ajili ya magonjwa yanayoweza kuukumba mmea na kudhoofisha ukuaji wake, hivyo basi wengi hushindwa kumudu gharama na kushindwa kutokana na upandaji wa bei.,
Vilevile kutokuwepo kwa uhakika wa masoko ya bidhaa za kilimo kwa bei inayoridhisha,unakuta mkulima anatumia gharama kubwa katika uzalishaji wa bidhaa lakini soko sio la uhakika na bei ya bidhaa inamuumiza mkulima,ukilinganisha na gharama kubwa alizozitumia katika uzalishaji, hivyo wengi kushindwa kufanya vizuri katika shughuli za kilimo.
Pia kukosekana kwa elimu ya kutosha juu ya pembejeo za kilimo, wakulima wengi hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya pembejeo kwa mfano mbegu, wengi hawafahamu ni mbegu zipi bora zinazoweza kustahimili katika udongo wa eneo Fulani, wengi hununua mbegu bila kupata ushauri wa wataalamu kutoka eneo husika,pia kwenye swala la uwekaji wa mbolea bado ni changamoto kujua mbolea ipi inafaa kuwekwa katika mazao kwa kipindi kipi katika ukuaji wa mmea, kukosekana kwa elimu ya kutosha husababisha wakulima wengi nchini kutopata matokeo mazuri yanayoridhisha kulingana na gharama wanazotumia katika uzalishaji.
Hivyo basi, Kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya dunia kuhakikisha kunakua na usalama wa chakula duniani, na ili kuhakikisha kilimo kinajikita katika biashara kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla, Serikali kupitia sekta ya kilimo na kwa kushirikiana na sekta binafsi inapaswa,
Kuweka utaratibu na usimamizi mzuri na ambao utakua endelevu ili kuhakikisha kwamba ruzuku ya mbolea ambayo serikali imeanza kutoa kuanzia Agosti 2022, inawanufaisha wakulima wote, na kuhakikisha wafanyabiashara wanauza mbolea kwa bei elekezi ya serikali ili kuwawezesha wakulima kuweza kumudu gharama za uzalishaji kutokana na unafuu wa bei ya mbolea. Pamoja na upatikanaji wa mbegu bora ili kumsaidia mkulima kupata matokeo mazuri.
Hata hivyo, serikali inapaswa kupanga na kudhibiti bei ya bidhaa za mazao pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya bidhaa, kwa namna ya kwamba bei ya bidhaa itakua rafiki kwa mkulima na pia kwa mnunuzi wa hali ya kawaida kiuchumi, haitamuumiza mkulima kulingana na gharama alizotumia katika uzalishaji na wala haitamuumiza mnunuzi.
Vilevile kuhamasisha wawekezaji katika sekta ya kilimo,utoaji wa mikopo kwa kuwagawia watu maeneo pamoja na pembejeo za uzalishaji wa kilimo ili kuhamasisha watu wengi Zaidi kujishughulisha na kilimo, kuanzisha mashamba ya pamoja(block farms) katika mikoa tofauti tofauti Zaidi ili kuwezesha na kusaidia ushiriki wa vijana katika shughuli za kilimo kwa maslahi ya taifa na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Aidha, ili kufikia lengo la serikali katika ukuaji wa kilimo cha umwagiliaji, kwamba kufikia 2030 asilimia 50 za shughuli za kilimo nchini kufanyika kwa njia ya umwagiliaji, serikali inapaswa kuweka utaratibu wa uvunaji wa maji ya mvua, kwani Tanzania kuna kiwango kikubwa cha mvua na tuna vyanzo vingi vya maji, kama serikali itaweka nyenzo ili vyanzo hivi vitumike katika kilimo cha umwagiliaji, itasaidia kuwa na uzalishaji wa kilimo endelevu na kufikia lengo la kilimo cha umwagiliaji.
Lakini pia elimu itolewe kwa vitendo kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya mbegu, mbolea, madawa na pembejeo zingine za kilimo ili kuleta matokeo bora katika sekta ya kilimo nchini.
Hivyo basi uhakika wa usalama wa chakula nchini na duniani kwa ujumla unategemea na mikakati,usimamizi na utekelezaji mzuri wa sera za kilimo ili kilimo kiwe na tija na kuleta matokea mazuri. Hii itasaidia kupunguza majanga mengine yasababishwayo na kutokuwepo kwa chakula cha kutosha(janga la njaa),ambalo linaathiri uzalishaji.

Upvote
3