Kilimo kinalipa? au niwaze mambo mengine!

ntita

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
513
Reaction score
285
wana jf salam.
mimi ni kijana ambaye nategemea kuingia mtaani siku chache zijazo(nipo kdt cha 6)

kati ya sekta ambazo nafikiria kuwekeza ni katika kilimo kwani baba alipoondoka ardhi ndo rasmali kubwa aliyoiacha.

kutokana na kwamba nililelewa dar nina ufaham mdogo sana kuhusu kilimo ndo maana imenibidi kuwauliza ndugu zangu ili nijue la kufanya mara tu ninapomaliza elimu yangu ya sekondari na nitakapokuwa naendelea na elimu ya juu.

mashamba hayo yapo mkoani kagera wilaya ya ngara hivyo anayefahamu kuhusu kilimo hasa kwa maeneo husika naomba unifahamishe ili nijue la kufanya,

natanguliza shukurani.
 
Ili uwe mkulima haswa uende sua ukasome agriculture general
 
Kinalipa ukitumia timing na mbinu za kisasa..., vuna hifadhi wakati wa msimu na uza wakati usio wa msimu (upate bei bora) tumia mbinu za kisasa na mbolea kuongeza mazao..,
 
Kilimo kinataka full participation na uwe na kipato kingine nje ya kilimo ili kukabili up and downs za kilimo. Kwenu Ngara kuna tatizo la manpower, migomba ndio hiyo inaliwa na ugonjwa, kahawa inayumba yumba ktk soko, sina hakika na kasheshe za Vanilla. Mazao mengine balaa liko ktk masoko huko kwenu. Sijui ardhi yenu ni kubwa kiasi gani, unaweza jaribu kufuga kienyeji wakati huu unaposoma.

Kama ungekuwa unaishi kule kule Ngara ningekushauri ukomae na kilimo, lakini kama utalima kwa njia ya simu, unaweza pata ugonjwa.
 
thanks mkuu.
 
Kulima c lazima uende chuo cha kilimo.kuna mabwana shamba bogas kabisa hawajui lolote wanafundishwa nawakulima wakawaida
 
kuna njia tatu za kupoteza pesa mwl wangu alinifundisha GAMBLING, AGRICULTURE NA WOMANIZER sasa sijui umejipanga kiasi gani kuwekeza
 
Hongera kwa mawazo ya kimapinduzi amini usiamini kilimo kinalipa sana alimradi tu usimamie kwa ukaribu sana ndio maana sasa wawekezaji wanakamata ardhi. Jaribu kuzalisha avocado pears grafted siku hizi zina soko kubwa sana hata nje kwani zinatumika pia kutengeneza product nyingi mbali na kuliwa kama tunda, kikubwa ni uzalishe kwa wingi
 
ubarikiwe.
 
Kilimo kinalipa sana hakuna biashara yenye ROI kubwa Kama Kilimo mkuu.Fanya utafiti utanambia kwa hili,hulipi kodi,pembejeo unauziwa bei Sawa na bure sasa si super profit hiyo Mungu akupe nini
 
Kilimo kinalipa sana hakuna biashara yenye ROI kubwa Kama Kilimo mkuu.Fanya utafiti utanambia kwa hili,hulipi kodi,pembejeo unauziwa bei Sawa na bure sasa si super profit hiyo Mungu akupe nini

asante mkuu, ngoja tumalizane na hii mitihan nijipange.
 
Karibu utatukuta tunaendelea na ushauri pia tutakupa
 
Dogo mawazo yko mazuri kilimo kinalipa kahawa na ndiz ni mazao yatakayochukua mda mrefu na utunzaji wahitajika...
Hakikisha unatumia kilimo cha kisasa
 
Kilimo kinalipa sana hakuna biashara yenye ROI kubwa Kama Kilimo mkuu.Fanya utafiti utanambia kwa hili,hulipi kodi,pembejeo unauziwa bei Sawa na bure sasa si super profit hiyo Mungu akupe nini

nimependa hapo kwenye kodi wakati wa kuvuna mteja anakuja shambani raha sana.
 
kuna njia tatu za kupoteza pesa mwl wangu alinifundisha GAMBLING, AGRICULTURE NA WOMANIZER sasa sijui umejipanga kiasi gani kuwekeza

Mwalimu wako ni bonge la kiraza na wewe kama bado unaamini hivyo Pole sana sitaki kusema wewe nawe ni nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…