KILIMO KWA MAENDELEO YA JAMII
Kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba, kilimo kinajumuisha mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama, ndege, nyuki, na uvuvi wa samaki. Kilimo ni uti wa mgongo kwa uchumi wa nchi zote zinazoendelea. Asilimia 95% ya vyakula, na mavazi tunavyotumia vinatokana na kilimo. Uchumi wetu unakua kila siku kutokana na wingi wa viwanda vinavyojengwa kila siku, viwanda hivyo vinategemea mazao (bidhaa) mbalimbali yanayotokana na kilimo, mfano viwanda vya kusindika nyama, viwanda vya kutengeneza mavazi kutokana na pamba na ngozi za wanyama, vivyo hivyo kilimo kinaleta ajira kwa vijana na watu mbalimbali.
Ili kuleta mabadiliko chanya kwenye nyanja ya kilimo, tunatakiwa tuzingatie haya;
Amani na usalama kati ya wakulima na wafugaji( kupunguza migogoro). Migogoro ya kila siku inayotokana na wakulima pamoja na wafugaji kwa asilimia kubwa inapunguza na kuondoa kabisa ufanisi na matokeo mazuri ya kilimo. Wakulima na wafugaji wanatakiwa wajue kwa asilimia kubwa wanategemeana ili kuleta matokeo mazuri bila kutumia nguvu kazi kubwa.
Pia tujaribu kuthibiti mabadiliko ya tabia nchi, mabadiliko ya tabia nchi yapo na husababishwa haswa na shughuli za binadamu. Hali hii itakayolazimisha watu kukabiliana na ruwaza mpya za hali ya hewa. Mkulima anatakiwa kufahamu kwamba kutozingatia masharti ya viuavijumbe na maradhi ndio chachu ya usugu wa dawa, kutumia viuatilifu bila maelekezo au uelewa kunaweza kuleta athari kwa kipindi cha baadae, tuzingatie ulimaji wa kupumzisha shamba (kilimo cha mzunguko) kwa mazao bora. Tupunguze uvuvi wa kutumia madawa kwani unapunguza na kuua samaki wadogo pia unapunguza ubora wa samaki
Ninaamini kuwawezesha wakulima hususani kwa kua na njia bora na nafuu za usambazaji pembejeo na kuanzishwa kwa Benki ya wakulima nchini itasaidia sekta ya kilimo kufika mbali zaidi, pia wakulima tujitahidi kuepukana na Imani potofu, kwa sababu asilimia kubwa ya mabwana shamba (maafisa ugani) ni wanaume ambao yumkini wakapigwa marufuku kuwasiliana na wakulima wa kike kutokana navikwazo vya kitamaduni licha ya kwamba wanawake wanafanya asilimia 70 (70%) ya wafanya kazi shambani.
Serikali iiangalie Sekta ya kilimo kwa jicho la tatu, kwa sababu, Sekta ya Kilimo inachukuliwa ndio sekta masikini ya watu wasiiosoma na waliokosa ajira kwenye sekta nyingine hivyo watu wapate Elimu wabadili mtizamo. Watanzania wanatakiwa wathamini na kukienzi kilimo waamini ni ajira kama ajira nyingine. Tunaiomba Serikali iongeze misaada kwa wakulima Kama vile pembejeo, wataalamu wa kutosha.
Pia iongeze miradi Kama vile Mradi wa kuongeza usalama wa chakula, kuendeleza miundombinu ya masoko pamoja na kuendeleza miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwa ufanisi. Serikali na taasisi binafsi itoe vipaumbile kwa vijana kwa kuwadhamini, (inawezakuwa kwa kutoa mikopo) wakipata sapoti (msaada) siku za mwanzo, msaada wa mtaji (eneo, pembejeo, madawa ) wataweza kuanzisha na kuendeleza miradi mbali mbali ya kilimo na ukawafaa kuchangia heshima na uchumi wa nchi pia kuukimbia umasikini kwa Sasa na baadae.
Serikali ipunguze tabia ya kuwazuia wakulima kuuza mazao mikoa au nchi jirani, kwa sababu hii inapunguza ubora wa masoko na biashara. Badala yake inatakiwa itoe kipaumbile kwa wakulima kuuza mazao mikoa na nchi jirani kwa kusaidia kutafuta masoko. Hii itasaidia kutoa motisha kwa wakulima kuongeza nguvu na juhudi za uzalishaji. Hata hivyo tunatakiwa tujitahidi kua na utaratibu mzuri wa kuhifadhi chakula cha kutosha kwa miaka kadhaa ya maadae dharura inapotokea haitotubabaisha sana.
Kingine tujitahidi sisi wenyewe kutengeneza mashine za kilimo kwa kuwatumia wahandisi wazawa na wale wasio wazawa. Hii itasaidia kujitosheleza kwa zana za kilimo ambazo mkulima wa kawaida ataweza kuzimudu kununua.
Sera ya Kilimo inatakiwa iwe ni ya kazi kwa maarifa na zana za kisasa na inayozingatia maswali ya elimu isiyo na mwisho, utafiti endelevu na maendeleo ya rasilimali watu wakati wote.
Mabwana shamba na mabibi shamba hawana utofauti na wakulima wengine huko kijijini katika kutokana na umaskini wao. Mabwana shamba na mabibi shamba hawapo vijijini kuwasaidia wakulima kuondokana na umaskini, Bali nao wameenda tena kutumbukia kwenye umasikini. Hii ni kwasababu Elimu na maarifa yao havitoshi. Hivyo ni lazima kuwepo na ofisi pamoja na shamba la kujifunzia, zana mbalimbali, gereji, madarasa ya kilimo, kitengo cha mbolea na umwagiliaji, nafaka pamoja na malighafi. Usafiri wa kuaminika kwa mabwana shamba pamoja na vitendea kazi. Wingi wa mabwana shamba hautakua na manufaa au matokeo chanya kama hakutakua na vitendea kaz pamoja na usafiri wa haraka unaoeleweka.
Tunaishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kilimo hadi kuweka siku ya kilimo Tanzania maarufu Kama Nane Nane. (Nane Nane ni sikukuu ya wakulima nchini Tanzania ambayo huwapa fursa wakulima, taasisi na wadau mbalimbali wa kilimo kote nchini kuonesha bidhaa zao na mafanikio yao katika mwaka husika.) Hi imeongeza mchango mkubwa kwa wakulima, kwasababu kupitia sikukuu hi wakulima wengi wanaitumia kuonyesha ujuzi wao na matokeo yao kwenye kilimo, pia wengi wao wananufaika kwa kupata wateja wa bidhaa zao, pia inasaidia kwa wale ambao walikua hawafanyi vizuri kwenye uzalishaji wakapata Elimu kwa wale ambao wamefanya vizuri.
Hivyo Basi kwa mtizamo wangu, ningependa kuiomba Serikali iweke hii siku hata Mara mbili kwa mwaka, ama sivyo basi ilazimike kuweka haya maonesho yaende kwa mizunguko fulani. Mfano Kama mwaka huu yatafanyika Kanda ya kaskazini Arusha Basi mwaka ujao yafanyike Kilimanjaro mwaka unaofuata yafanyike Manyara. Hii itasaidia ata kwa wale wakulima masikini (wasiokua na uwezo wa nauli ya kufika Arusha) waweze kushiriki kwenye mkoa wao.
Kwa kumalizia kilimo kina kinamanufaa mengi kwetu, hasa tukizingatia yote niliyoyaorodhesha hapo juu. Tunaiomba Serikali itoe misaada mbalimbali kama vile isaidie kutoa Elimu kwa wananchi wake. Elimu ilenge faida za kilimo hasa tukilima kwa kufuata utaratibu mzuri, pia Serikali itoe hari kwa wakulima kuwapa ushirikiano mzuri mabwana shamba.
(Ushirikiano ni muhimu kwa wote Serikali- Mabwana shamba- Wakulima) hii italeta matokeo mazuri, tukumbuke wahenga walisema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hivyo hivyo kidole kimoja hakivunji chawa. Serikali imchukulie mkulima kama muwekezaji kwa sababu tayari ana ardhi ambayo inathamani na pengine mazao kadhaa ya kudumu. Kufumba na kufumbua tutamkomboa mkulima na umasikini, hapo hapo taifa litakua likijiendesha kichakula na kibiashara.

Upvote
0