Kilimo kwa njia ya greenhouse

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Posts
872
Reaction score
141
Wakuu ninaomba ushauri wa nini hasa napaswa kukifanya ili mradi wangu uwe na tija na ufanisi ili kupata matokeo ninayoyatarajia.

Iko hivi:

Baada ya kuchunguza hali halisi ya ajira kwa vijana wanaomaliza elimu kwenye vyuo vya elimu ya juu hapa nchini, nimegundua jambo moja lililo dhahiri kuwa vijana wengi hupambana na wengi wao kushindwa kupata ajira.

Nikiri wazi pia kuwa ukosefu huu wa ajira unasababishwa kwa kiasi kikubwa na vijana hao kutegemea kuajiriwa zaidi badala ya kuangalia njia rahisi za kujiajiri na kujikwamua kimaisha.

Sasa nimeamua, nimeona ni bora nijiingize kwenye shughuri ya kilimo ambayo ndiyo ajira rahisi zaidi ikilinganishwa na masoko mengine.

Baada ya kuangalia pia aina ya kilimo ambacho haswa kitaendana na kipato changu kidogo nilicho nacho, nimeona nibora nifanye mazao ya muda mfupi ambayo yatafanya niwe ya fedha angalau kila baada ya miezi miwili.

Katika kuangalia aina ya mazao hayo nimeona kilimo cha nyaya ndicho chenye kipato cha uhakika ikilinganishwa na mazao mengine ambayo kwanza utokaji wake sokoni ni mdogo na vipato ni vidogo pia.

Kwa ufupi iko hivi, kilimo cha nyanya nilichoona kinanifaa na kunihakikishia kipato katika mwaka ni kwa kutumia indoor agriculture (greenhouse).

Naombeni ushauri wenu wa kitaalamu juu ya mahitaji ninayopaswa kuwa nayo ili kuukamilisha mradi huu. Mwenye uzoefu pia anipe gharama za ujenzi wa nyumba. Nahitaji kujua kuhusu masuala ya soil pH, mbolea ninayotakiwa kwa huu mradi, nk nk.

Please wadau nipeni mkono wa shirika
 
Kuna mdau mmoja alituletea picha za Green House yake ipo Kibaha nadhani labda akija yeye anaweza kutufungua macho
 
Tafuta post moja imo humu ndani utafunguka macho zaidi andika neno green house
 
Nivea hiyo post mbona haionekani mkuu? Wengine pia tungependa kupta hiyo ilimu ili tujikwamue kimaisha,

kama unaweza pata link ya hiyo mada au thredi basi tupia humu mkuu,

hata hivyo namshukuru muuliza swali au muanzisha thread kwani majibu yakipatikana tutapata faida wengi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ipo hivi...,

Greenhouse ni kwamba unatengeneza mazingira bora ambayo yanafaa kwa zao unalolima (which means additional cost) kama kuna baridi sana au hakuna jua unaweka artificial lights na heaters, lakini ukiona hii nchi yetu imebalikiwa na a natural greenhouse (climate sio mbaya na vitu vingi vinaota bila umuhimu wa greenhouse)

Kwahio utaona kwamba unless zao unalolima lina value kubwa sana na wewe unaweza kuuza kwa bei nafuu kuliko competition (na hii ni baada ya ku-cater additional cost za running greenhouse) basi endelea, au kama unaweza kulima zao out of season (yaani wakati wengine wanashindwa kulima, au mazao ambayo huku sio mengi kama strawberries n.k.) value products, kwa kukusaidia ngoja nikupe list ya Top Ten Profitable Plants kwa mtu mwenye eneo dogo (ila hii sio kwa soko letu kwahio do your homework)

The top 10 most profitable plants to grow in your garden (Vegetable, USD Value/SF):

  1. Cilantro - $21.20
  2. Arugula-Roquette - $20.92
  3. Green Salad Mix - $17.55
  4. Chives - $16.40
  5. Dill - $16.40
  6. Lettuce - $16.20
  7. Tomato, Cherry, small & medium - $15.57
  8. Turnip - $9.90
  9. Tomato, large - $9.50
  10. Squash, Winter - $8.40
Top 10 least profitable plants to grow in your garden (Vegetable, USD Value/SF):

  1. Eggplant - $1.10
  2. Greens, Mustard $1.10
  3. Rutabaga - $1.00
  4. Beet - $0.89
  5. Cabbage, Savoy - $0.80
  6. Broccoli - $0.80
  7. Kohlrabi - $0.75
  8. Cauliflower - $0.60
  9. Broccoli, Chinese - $0.60
  10. Cabbage - $0.50

Source: The Most Profitable Plants for Your Garden | Apartment Therapy
 
Kwa upatikanaji wa green house cheki na jamaa wa Balton
Kwa mambo ya soil PH na mbolea peleka sampuli ya udongo wako SUA watakusaidia kuupima na kukushauri juu ya aina ya Mbolea na kamaa shamba lako linafaa au vp
 
sina uhakika lakini nasikia cost yake kila kitu mpaka inakuwa tayari inaweza kufika mil 4-10 inategemea na size ya nyumba hapa TZ ulizia balton wako Arusha, Dar na Iringa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…