Daniel Anderson
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 872
- 141
Wakuu ninaomba ushauri wa nini hasa napaswa kukifanya ili mradi wangu uwe na tija na ufanisi ili kupata matokeo ninayoyatarajia.
Iko hivi:
Baada ya kuchunguza hali halisi ya ajira kwa vijana wanaomaliza elimu kwenye vyuo vya elimu ya juu hapa nchini, nimegundua jambo moja lililo dhahiri kuwa vijana wengi hupambana na wengi wao kushindwa kupata ajira.
Nikiri wazi pia kuwa ukosefu huu wa ajira unasababishwa kwa kiasi kikubwa na vijana hao kutegemea kuajiriwa zaidi badala ya kuangalia njia rahisi za kujiajiri na kujikwamua kimaisha.
Sasa nimeamua, nimeona ni bora nijiingize kwenye shughuri ya kilimo ambayo ndiyo ajira rahisi zaidi ikilinganishwa na masoko mengine.
Baada ya kuangalia pia aina ya kilimo ambacho haswa kitaendana na kipato changu kidogo nilicho nacho, nimeona nibora nifanye mazao ya muda mfupi ambayo yatafanya niwe ya fedha angalau kila baada ya miezi miwili.
Katika kuangalia aina ya mazao hayo nimeona kilimo cha nyaya ndicho chenye kipato cha uhakika ikilinganishwa na mazao mengine ambayo kwanza utokaji wake sokoni ni mdogo na vipato ni vidogo pia.
Kwa ufupi iko hivi, kilimo cha nyanya nilichoona kinanifaa na kunihakikishia kipato katika mwaka ni kwa kutumia indoor agriculture (greenhouse).
Naombeni ushauri wenu wa kitaalamu juu ya mahitaji ninayopaswa kuwa nayo ili kuukamilisha mradi huu. Mwenye uzoefu pia anipe gharama za ujenzi wa nyumba. Nahitaji kujua kuhusu masuala ya soil pH, mbolea ninayotakiwa kwa huu mradi, nk nk.
Please wadau nipeni mkono wa shirika