Kilimo na biashara ya mkonge/ katani Tanzania

Kilimo na biashara ya mkonge/ katani Tanzania

Habari wanajamii forum ,mimi ni mdau wa muda mrefu sana ndani ya forum hii lakini nikiwa kama msomaji tu, kupitia forum hii nimejifunza mambo mengi, nimecheka na kufurahi, pamoja na kuelimika kwenye baadhi ya mambo ambayo sikuwa nayaelewa vizuri hapo mwanzo.

Lengo kuu la kuleta huu uzi kwenu ni kutoa elimu na maarifa sahihi kuhusu kilimo na biashara ya mkonge/katani hapa tanzania kwa maana mimi ni mfanyabiashara mdogo wa kati wa mkonge, hivyo basi kwa uzoefu na maarifa yangu kuhusu zao hili nimeamua kuandaa hii taarifa ili kuleta uelewa mzuri zaidi.

Nimeanda hii doc (pdf) ikiwa inaelezea na kufafanua kwa uzuri nini maana ya mkonge, kilimo cha mkonge kiujumla na jinsi pesa inavyopatikana kwa ngazi zote ndani ya biashara ya mkonge, ndani ya maelezo hayo pia nimeambatanisha na picha mbalimbali ili kuleta uelewa mzuri wa nini halisi kinaelezwa.

Kwa yeyote aliye na uzoefu na taarifa za ziada kuhusu mkonge anaweza kuongezea, kushauri, kukosoa na pia kuleta ushuhuda unahusiana na mkonge, lengo kuu likiwa ni kujenga uelewa nzuri zaidi wa kilimo na biashara ya mkonge kwa watanzania.

Asante [emoji120]

Note:
A) Kama kuna tatizo lolote la kiuandishi ndani ya doc basi tuvumiliane na tusameheana kwenye hilo.

B) Nimetumia ID mpya kwa sababu zangu binafsi (naomba tujikite kwenye lengo la uzi).

View attachment 2965517
hongera sana mkuu nami nimeingia kwenye kilimo nimepanda eka 62 ina mwaka sasa inshaAllah tuombe uzima..but hiyo attachment haifunguki kwangu
 
Kuna michepuko yangu ya zamani imehamia tanga huko. Pangani.
Kumbe ina hela.ngoja niwapige mizinga.
 
Kazi nzuri Sana.Kama kuna group la WhatsApp la Value Chain ya Mkonge tushirikishane Nina Wadau wangu Wanalima Mkonge Handeni watajoin.
 
hongera sana mkuu nami nimeingia kwenye kilimo nimepanda eka 62 ina mwaka sasa inshaAllah tuombe uzima..but hiyo attachment haifunguki kwangu
Umepanda kwa mara moja? Umejiandaaje kwa ajili ya usafi? Una tractor lenye slasher? Au boom sprayer kwa ajili ya herbicides? Kumbuka kazi kuu palizi.... ukitegemea manpower lazima udate
 
Umepanda kwa mara moja? Umejiandaaje kwa ajili ya usafi? Una tractor lenye slasher? Au boom sprayer kwa ajili ya herbicides? Kumbuka kazi kuu palizi.... ukitegemea manpower lazima udate
Nina ekari Mia this time nina panda mbegu nije nihamishie,vipi kuhusu palizi mnafanyaga nini kurahisisha
 
Mungu akutunze mkuu. Nimeongeza kitu kikubwa
 
Nina ekari Mia this time nina panda mbegu nije nihamishie,vipi kuhusu palizi mnafanyaga nini kurahisisha
Kama uwezo wako ni mdogo anda kupanda chache chache sije ukaupoteza shamba, palizi hutegemea na ulipo na namna ardhi inavyofanya ila mkonge mdogo unapaliliwa kama mahindi tu angalau ukifikisha miaka 2 unaweza anza fyekea tu
 
Kuna mdau ameniambia madalali kwenye soko la mauzo Wana Rudisha nyuma wakulima, wanakuibia Sana kiasi wao ndio Wana tajirika
 
Umepanda kwa mara moja? Umejiandaaje kwa ajili ya usafi? Una tractor lenye slasher? Au boom sprayer kwa ajili ya herbicides? Kumbuka kazi kuu palizi.... ukitegemea manpower lazima udate
nimepanda kwa mara moja shamba lote na palizi nafanya kwenye miraba kwa mkono uzuri nipo karibu na estate ya METL so nguvu kazi napata kupitia hapo na kwa sasa narudia mbegu ambazo hazijakaa vizuri nimejipanga kaka Alhamdulilah
 
Hongera sana mkuu,endelea kutupa updated tuzidi kuimarika km darasani
 
Back
Top Bottom