Kilimo na TEHAMA yewe masomo ya lazima shuleni

Kilimo na TEHAMA yewe masomo ya lazima shuleni

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Kwa kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu na kinachangia 80% ya pato la Taifa, ni vyema Serikali ikalifanya somo hilo kuwa la lazima ngazi zote za shule.

Pia kwa upande wa TEHAMA tunaona jinsi ambavyo dunia inakimbia kwenda kwenye mapinduzi ya Kiteknolojia na ndio msingi wa maendeleo wa kila sekta duniani kote, ni muda muafaka sasa serikali iingize kama somo la lazima kuanzia ngazi ya chini.

Masomo mengine kama Hisabati, Uraia, Kiswahili na Kingereza nayo ni ya muhimu ili kuzalisha watu watakaotoa mchango wa mabadiliko ya moja kwa moja kwa taifa na kuongeza wigo wa ajira.
 
Back
Top Bottom