Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Mnapouliza maswali jaribuni kuwa waungwana, porojo za social media zinatoka wapi? Kuna ajabu gani hapo? Mbona hayo mavuno ni ya kawaida kwanza nipo chini ya malengo.
Mkuu asante kwa yoote. Ila je unaponunua mbegu kutoka kenya pale mpakani hawazikamati kwa sababu mbegu na madawa ni lazima yathibitishwe na mamlaka husika.
Kama inawezekana naomba nitumie mawasiliano inbox, na mimi nipo kwenye project ya mahindi na tunatumia mbegu kutoka kenya seed co.
 
Ni kweli kilimo kinalipa sana, naandaa mtaji wa milion 3 nataka nizipeleke shambani, kwa sasa naanda business plan lakini kazi yangu serikalini siachii...kilimo kitakuwa ni nyongeza tu basi

Mkuu wengi wa walioingia hasara katika kilimo ni wale wako ofisini kisha wanaagiza watu wawalimie. Hebu kwenye kilimo hesabu ni kosa namba moja, hiyo lazima ile kwako.
 
Mkuu wengi wa walioingia hasara katika kilimo ni wale wako ofisini kisha wanaagiza watu wawalimie. Hebu kwenye kilimo hesabu ni kosa namba moja, hiyo lazima ile kwako.
Sasa waofisini mnatushauri tufanyeje na tunapenda kilimo sanaa...?
 
Bulaza Molembe nakuunga mkono 100%, najiandaa kukodi ekari 5 nilime mpunga mcmu huu.....nitarudi hapa mwakani kutoa mrejesho, Mungu Muweza wa yote akitujalia pumzi ya uhai!
 
Ukitaka kufanikiwa lazma uwe risk taker, wengi wanashindwa kutoka wakiogopa risk tena hasa kw maneno ya watu wanaovunja moyo.Utamu wa ngoma ingia ucheze!
 
Haya ndo mawazo ya mcng, co vijana tunajifanya research research watu wanatusua....jiulize wakulima kule kijijini wamelima kuanzia enzi hizo tena bila njia bora za kilimo lkn wamemudu maisha na kuwasomesha watoto hadi vyuo vikuu, leo una-graduate unajifanya hulimi hadi ufanye research![emoji57]
 
Bro, em acha kuzidisha ugumu wa maisha....we umeandika b'nss plan ngapi na bank gani imekupa loan nami niandike!? Mabenki yamekuwa yanajinadi tu ila ktk uhalisia pesa ya bank kuipata kw style hyo ni ngumu sana!
 
Kila kilimo sio lazima ukakope, hivi kijana aliyemaliza chuo kikuu atashindwa kupata laki 5 akaanzisha kilimo, mimi nakumbuka kipindi nipo chuo nilikuwa natunza pesa kila boom nimemaliza nina zaidi ya milioni moja.
Hii ndo akili
 
Kitu chenye pesa na mafanikio hakifanywi na kila mtu mkuu! Ingekua hivyo kila mtu angekua tajiri
Na lazma uwe na moyo wa chuma km yule raia wa England aliyetabiri Leicester FC wangebeba kombe EPL mcmu ulopita lkn leo hii ni billionea, vingnevyo utasubiri sn!
 
Mkuu mimi nalima katesh na Tanga. Katesh haipungui 40 kwa heka wakati Tanga ni 50. Mkuu ni kweli ni bei za tractor mnazungumzia au ni ng'ombe na punda?
Tanga sehemu gani mkuu?
 
Kilimo cha umwagiliaji may be chamvua hiki chaweza kukuliza
 
Mkuu ninakupongeza kwa hatua uliyopiga. Lakini bado sijaridhika na gharama ulotaja, ninasema hivyo kwa kuwa mimi pia nimewekeza kwenye kilimo cha mahindi kwa miaka mitano sasa. Naomba utuoneshe mchanganuo wa gharama zifutatazo:

*Kukodi kila heka 50,000.
*Kulima kila heka sh. ngapi?
*Palizi kila heka sh. ngapi
*Mbegu sh. ngapi kila kilo?
*Kilo ngapi za mbegu kila heka?
*Kuvuna sh. ngapi kila heka?
*Kupanda sh. ngapi kila heka?
*Kupukuchua sh ngapi?
Then tuzidishe mara mbili, pia utuambie wastani wa mavuno kwa heka ni gunia ngapi na uliuza kwa bei gani?

Ni vizuri kuhamasisha watu lakini si kwa kuwadanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…