Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Msidanye watu KILIMO kina changamoto nyingi kuanzia kulima hadi kuuza baada ya kuvuna
 
Kilimo ndo mpango mzima
Sasa mi nataka kulima ila mbegu sina waweza kuniazima kama tani moja hivi
 
Mwaka Jana nimelima heka moja ya vitunguu na jumla gharama nilitumia 1,700,000/= nikafanikiwa kupata gunia 72 ambayo kila gunia niliuza kwa 90,000/= sawa na tsh 6,480,000/= ukitoa gharama zangu unapata baki ya tsh 4,780,000/= Nilipotoa gharama zangu zote nyingine kama usafiri na chakula nilipokuwa shamba nikabakiwa na 4,300,000/= Nilitumia miezi minne mpaka kuvuna na approximation ni kama kila mwez niliingiza 1 million. Ni kiasi kidogo na ni kikubwa pia.
Tujifunze kuwekeza shambani

Mkuu naomba nisaidie namba yako ninahitaji kulima kitunguu mwaka huu.
 
KILIMO cha kitanzania bado kina changamoto nyingi sana
Tatizo kubwa tulilo nalo nikupenda kujaribu kuliko kufanya ili tufanikiwe ndio maana utakuta mtu mmoja anapost katika wall kuwa kilimo kinalipa hata picha ya Shamba lake usiweze kuiona ukimuuliza mbinu alizotumia katika ukulima wake kwa kulima heka mbili hana majibu sahihi kama mbashiri wa nyota

Kuna watu wa kweli na ni wakulima kweli wao wanazijua vilivyo changamoto zilizopo ktk KILIMO

Mkulima unapoonza kulima kwa mala ya kwanza usitegemee faida unaweza kutumia laki tano na ukavuna pesa isiyozidi laki moja uspokuwa jasiri hauwezi kurudi shambani

Pia kuna changamoto katika ardhi zetu sio kweli kila eneo linafaa kwa kilimo cha mahindi kama mleta post anavyo jaribu kutuhadaa kuna maeneo mengi hapa nchini mahindi hayawezi kustawi kabisa hata ulime kwa mbolea kutoka mbinguni

Pia kuna aina na aina za mbegu ambazo ni sahihi kulingana na sehem husika hasa katika mbegu za mahindi kuna mbegu ambazo ukizipanda katika maeneo furani hazioti au zitaota lakini zinaishia kuwa super tool hazitoi hata mbele wele

Mimi binafsi ni mkulima natambua vilivyo changamoto zilizojaa shambani kabla haujajaribu kuanza KILIMO Fanya research kuhusu KILIMO unacho kikusudia kuanzia hatua za awali hadi utakapo vuna
Naamin kila kijana wa kitanzania angependa kulima kuliko kutumikishwa lakini changamoto ambazo wakulima wanakutana nazo kimekuwa ni kikwazo kikubwa katika sekta hiyo

Mimi nashauri tutumie fursa ya mitandao kupiga kelele kuhusu changamoto za KILIMO ili watu waweze kuzitafutia ufumbuzi kuliko kusema mafanikio pekee huku tukificha ukweli chini ya carpet
 
Kuweni makini kuna watu sio wa kweli hata Kama Ni rafiki yako. Ekari moja ya kitunguu itoe gunia 113?!! Na bei ya shambani 90,000!! Usije kuja kuwa disappointed. Mwambie aseme ukweli maana kuna watu hawataki kuonekana kuwa wamepata hasara

Inategemea na timing ya soko sio kulima tu msimu wowote. Kitunguu kinaweza kutoka mpaka gunia 200 kwa mbegu ya hybrid sema vitunguu vyake ni vikubwa sana.
 
Kuna misimu ambayo ni mizur na ina hela saana lkn gharama za uendeshaji wa shamba ni kubwa lkn pia na faida utakayopata ni kubwa pia msimu wa mvua yan kuanzia November mpka may huu msimu ni mgumu kwa vitunguu katika maeneo meng kwasbb ya mvua na barid gharama za uendeshaji kwa heka inaweza fika 3ml na kuzid kwasbb ya ununuz wa dawa za ukungu n.k pia unaweza ukapiga dawa heka zima baada ya muda hata dawa haijafanya kazi mvua inanyesha kwhyo inabid urudie dawa changamoto ni nying msimu huu lkn kwenye mauzo pia huwa mazur gunia hufika had lak 200 na ukifata masharti unapata mavuno mazur ukilinganisha na misimu mingne gharama ya uendeshaji inakuwa ya kawaida lkn na bei ya mauzo pia huwa ya kawaida
 
Kujifanya mnajua research sana ndo kunawafanya muwe maskini. Watu wanaongelea ushuhuda bado unataka afanye research tena theoretically??? Ili approve nini wakati tayari ameshafaya pratically??

Tatizo letu vijana tunakuwa sio risk takers! Na lazima tujue the mkre risk you take the more reward you are likely to get!

Sasa mkikutana na waoga kama jawa wanaoogopa kuthubutu na mkawasikiliza mtajikuta mnazeeka maskini na sio katika kulima tu, katika kila biashara watu wa namna hii wapo. Mtu anakwambia mimi nina boda boda yangu na napiga hela kiasi flan kwa mwezi, badalaya kumuuliza unafanye upate hela kama hiyo unaanza kumwambia pikipiki nikinunua itapata ajali! Hawa watu wa type hii ni wa kupuuzwa kabisa!

Mimi nawahakikishia hela ipo kwenye kilimo na ni uhakika sana. Ukichemka msimu wa kwanza msimu ujao unatusua. Cha msingi ni kuwauliza wanaofanikiwa wanapitia njia zipi na sio kuwaambia ukilima mazao yatakauka mvuahaitanyesha.

Achamaneno andaa shamba alafu uvune tuone yakikosa soko sasa!
Umenikuna
 
Wat u say s ver true mm nmemaliza chuo mwaka juz mwaka jana may nikabahatika kupata ajira mbeya serikalin lkn baada ya muda tulisimamishwa kupisha ukaguz wa wafanyakazi hewa na sasa ni mwaka unaenda hatujarudishwa kazin lkn kule mm nilikutana na fursa ya kilimo cha vitunguu huwez amin nilichangamkia fursa sasa hiv ninavyoongea nakaribia kuvuna na nahisi kilimo ndo kazi yang sitaaka tena ajira
66c7cfb2deb91f6380a540df5095b90c.jpg

Naomba mawasiliano yako mkuu. Nina mpango wa kulima kitunguu.
 
WAJINGA NDIO WALIWAO NANI KAKUAMBIA BOOM LINATOKA KILA BAADA YA MWEZI KAFANYE TAFITI URUDI UPYA
Okay. Naona unamawazo madogo sana na unafikiria kwamba mpka upate makubwa ndio ujihesabie umejipanga hii itakusumbua sana.

Mwanachuo aliye weza kupata bahati ya kupata boom anapewa boom mara mbili kwa semester ya miezi 4 kwahiyo ni kila baada ya miezi miwili.

Sasa basi mwanachuo huyo mwenye bahati yakupata mkopo kila baada ya miezi miwili ambapo atapata 500,000 tuseme achana na 700,000 atakayo pewa semester ya kwanza awamu ya kwanza ya boom hilo, igawanye 500,000 kwa miezi miwili itakuwa 250,000 kwahiyo katika pesa hiyo akiweka 20,000 tuu kiwango cha kawaida kwa miezi minne atakuwa na 80,000. Kwa mwaka ataweka 160,000, kwa miaka mitatu atakuwa na 480,000. Sasa kwa pesa hii unaniambia bado hajaweza kuanza na kitu chochote baada ya masomo yake?

Tuache kubisha tuu ilituonekane tumebisha na tumeandika kitu waza vyema ndio tupate hoja za kusimamia. Itatusaidia sana kutatua matatizo yetu binafsi na ya jamii kwa ujumla.

Uwe na siku njema.
 
Wat u say s ver true mm nmemaliza chuo mwaka juz mwaka jana may nikabahatika kupata ajira mbeya serikalin lkn baada ya muda tulisimamishwa kupisha ukaguz wa wafanyakazi hewa na sasa ni mwaka unaenda hatujarudishwa kazin lkn kule mm nilikutana na fursa ya kilimo cha vitunguu huwez amin nilichangamkia fursa sasa hiv ninavyoongea nakaribia kuvuna na nahisi kilimo ndo kazi yang sitaaka tena ajira
66c7cfb2deb91f6380a540df5095b90c.jpg
Uko wapi mkuu! Mana nami Niko MBEYA pia!

Mwaka jana nimelima kitunguu USANGU ila hakikufanya vizuri kabisa, ila sijakata. We umelimia sehemu gani....vp ninaweza pata shamba wakati gani!??
 
Uko wapi mkuu! Mana nami Niko MBEYA pia!

Mwaka jana nimelima kitunguu USANGU ila hakikufanya vizuri kabisa, ila sijakata. We umelimia sehemu gani....vp ninaweza pata shamba wakati gani!??
Mm nmelima Mbeya sehemu inaitwa ilongo mashamba yapo muda wowote especially kipindi hiki watu wanakaribia kumaliza kuvuna mahindi yao
 
Kuna ndg yangu moja alinambia ukiwa unasoma na kufikiria zaid kuajiriwa huna tofaut na mtu anaejiandaa kufeli, lkn pia alinambia kusoma Sana bila mpangilio wa maisha ni kukwepa mafanikio na wengi walothubutu kuwekeza bila kuhofia hasara ndo walofanikiwa na akanambia vijana wengi vijijini wanafeli maisha ni kwasababu wanajikita kwenye kilimo baada ya kuwa na majukumu na hawaamin kuhusu kilimo ispokuwa wanaamin Katka kusoma na kupata ajira kitu ambacho wanakosa kwasababu mbali mbali za kifamilia au binafsi na ndo mana hawako siriazi na kilimo na ukija upande wa wengi walosoma soma hawahisi kilimo kama kinanyanyua kwasabab hawaoni mafanikio kwa waliojikta kwenye kilimo ambao ndo nao hapo juu kwahyo ndo mana humu ndani kumekuwa na mabishano kdgo.. Nakumbuka primary kulikuwa na habar flani Hv hapa ntaiandika kwa kifupi sina kumbukumbu vzuri "karudi Baba mmoja toka safari ya mbali kavmba yote mapaja na kutetemeka mwili , watoto Wake wakaja ili kumtaka hali, wakataka na kauli iwafae maishani, Mzee akawajibu kwamba baba yenu ninaumwa hapa nilipo sina hali, kama mnataka Mali mtaipata shambani. Mimi ni miongoni mwa vijana wanaoishi kijijin na nipo nimejkta kwenye kilimo kwa Mara ya kwanza tangu nihtimu ngazi ya stashahada mwaka Jana baada ya kuona mafanikio ya vijana wenzang ambao nao waliamua kujikta kwenye kilimo na tunalima kilimo cha kawaida tu huku tukitarajia kukiadvance siku zijazo.. Karbuni sana wasomi mbalimbali ambao mmekosa ajira na naamin hamtataman kuajiriwa..
 
Naunga mkono hoja yako kuwa utafiti wakati mwingine unatisha wala ila ni muhimu kama una muda kufanya utafiti has wa masoko. Kilimo inalipa sana, mimi nililima hekari nne za nanasi Mwavi Kiwangwa baada ya kuona faida nikaamgua nilime hekari 22. Ndani ya shamba hilo kuna minanasi kama 500,000, ilianza kuzaa kidogo mwaka jana ila mwaka huu na hali ya mvua inavyoendelea nategemea kuvuna si chini ya nanasi 200,000, piga hesabu mwenyewe kwa bei yako mwenyewe ni kiasi gani hapo. Twende kilimoni.
Kujifanya mnajua research sana ndo kunawafanya muwe maskini. Watu wanaongelea ushuhuda bado unataka afanye research tena theoretically??? Ili approve nini wakati tayari ameshafaya pratically??

Tatizo letu vijana tunakuwa sio risk takers! Na lazima tujue the mkre risk you take the more reward you are likely to get!

Sasa mkikutana na waoga kama jawa wanaoogopa kuthubutu na mkawasikiliza mtajikuta mnazeeka maskini na sio katika kulima tu, katika kila biashara watu wa namna hii wapo. Mtu anakwambia mimi nina boda boda yangu na napiga hela kiasi flan kwa mwezi, badalaya kumuuliza unafanye upate hela kama hiyo unaanza kumwambia pikipiki nikinunua itapata ajali! Hawa watu wa type hii ni wa kupuuzwa kabisa!

Mimi nawahakikishia hela ipo kwenye kilimo na ni uhakika sana. Ukichemka msimu wa kwanza msimu ujao unatusua. Cha msingi ni kuwauliza wanaofanikiwa wanapitia njia zipi na sio kuwaambia ukilima mazao yatakauka mvuahaitanyesha.

Achamaneno andaa shamba alafu uvune tuone yakikosa soko sasa!
nU
 
Back
Top Bottom