Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Wala sijaja kufuata consultation humu, huku kwetu kuna watu wanaitwa "Bwana/Bibi Shamba". Wewe naona ndiyo unatoa online consultation ya kujitolea!
Hahaha una wasiwasi sana mkuu, me mkulima tu kama wewe.
 
Uko sawa kabisa mkuu, huu ndo ukweli ingawa waliowengi hawaelewi hadi iwatokee puani.

Kuna nyanya zilioza morogoro mwaka jana kwa kukosa soko.
Hii ni dalili ya kutojua consumer atapatikana muda gani.
 
Hahaha kuna watu ukiwaambia ukweli wanavimba wanataka kusifiwa wakati uhalisia wa kilimo chetu uko ivo, tunalima kupata chakula.
 
Umwagiliaji si lazima iwe drip kama ulikalilishwa, kuna furrow mkuu pia inatumika.

Najua historia ya kilimo na mafanikio yake kwa hizo nchi huijui ila ubishi tu umekujaa.
Kwenye mashamba makubwa ya Urusi na baadhi ya majimbo ya USA ukiisha msimu wa kilimo huwa ni msimu wa baridi kali tofauti na kwetu huku ambako huwa ni joto kali na ukame, kule wao waga wanatunza msosi kwa ajili ya mifugo yao tofauti na kwetu na baadhi ya mazao tu kama ngano ndo huimili kipindi hiki lakini mahindi, zao kuu la USA hulimwa kipindi chenye mvua hicho cha kutunza maji ya mvua ni kwenye baadhi ya majimbo mfano Carlifonia ambako hakulimwi mahindi.
 
Hahaha kuna watu ukiwaambia ukweli wanavimba wanataka kusifiwa wakati uhalisia wa kilimo chetu uko ivo, tunalima kupata chakula.
Bwana dab hapa umechangia vyema ni kweli bongo hatulimi kibiashara kabisa na hii kujisifu huku unaonesha jisi gani tulivyo mafukara
 
Ardhi inakodishwa mkuu nenda hata Uyole mjini utakodisha mashamba ya viazi na kabeji uporoto au kawetere bei chee, after all mashamba sehemu nyingi ni ya kukodisha mkuu,usiogope
Mkuu, hibi kwa maeno ya uyole ba ule ukanda wanaolima viazi mviringo kama unaenda tukuyu , bei za mashamba ya kukodi zinarange vipi /hekari?
Kama wajua
 
Hahaha kuna watu ukiwaambia ukweli wanavimba wanataka kusifiwa wakati uhalisia wa kilimo chetu uko ivo, tunalima kupata chakula.
ukweli ndo huo,kilimo kinamlipa dalali lakini sio mshika jembe,watu tulishajaribu huko ufuta,mahindi tikiti lakini waaap,anayeongeaongea kuhusu kilimo hapa haelewi anachozungumza
 
Mkuu, hibi kwa maeno ya uyole ba ule ukanda wanaolima viazi mviringo kama unaenda tukuyu , bei za mashamba ya kukodi zinarange vipi /hekari?
Kama wajua
Inategemea mkuu mashamba yaliyo barabarani bei ya pango iko juu kidogo ukilinganisha na mashamba ya ndanindani mbali kidogo na barabara but kule Ntangano na Uporoto juu bei inarange Laki hadi Laki Mbili kwa Mwaka
 
Acheni ubahili kenge nyinyi kilo moja kitu gani kwa watu wawili tena wanaofanya kazi ngumu

sasa ''ukenge'' wetu unakuja vipi hapa mkuu?? it was just a joke mi mwenyewe kila moja ya unga nakula milo miwili na nusu..

TIP:
i think your a great thinker in here so learn to avoid the use of abusive language.
Gracia
 
its ok if it was a joke am sorry man, kawaida huwa sipendi kuona watu wanavyowanyonya manual laborers ujira mdogo sasa hata chakula jamani napo mnawabania
 
Napenda sanaa kuwekeza katka kilimo....nmeshajaribu kulima matikiti mara mbili nikakosa......nataka nijaribu kwingne
 
Acheni ubahili kenge nyinyi kilo moja kitu gani kwa watu wawili tena wanaofanya kazi ngumu

Mkuu inaonekana hufamu unalolizungumza. Labda ungekuwa mkulima ungejua nasema nini. Kumbuka mkulima anakutana na gharama kubwa katika pembejeo nk ila sokoni analaliwa sana na inaonekana kama hakuna suluhisho la hili. Sasa iwapo vijana wawili watakula kilo moja ya unga kwa mlo mmoja, huoni watakuwa wanazidisha gharama ya uzalishaji ambayo soko sio rafiki hivyo?
 
Sasa mkuu nn kifanyike? Wasipo shiba sasa watafanyaje kazi?
 
Kuuliza sio vibaya. Kuna watu mimi nafahamu wamelima na wamepoteza hela au kurudisha walichowekeza tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…