Watu wanasema kilimo kigumu yeah hakuna urahisi kwenye kutengeneza pesa
Iko hivi ukiamua kufanya kilimo ni kama biashara panda shuka hazikosekani
Kuna msimu mtu anaweza akawa ameanza kilimo akavuna akakuta bei sokoni ni nzuri. Kundi hili kwa mfano msimu ujao soko likiwa na bei ndogo ndio huwa wanajazana mitandaoni na kusema kilimo hakilipi hakieleweki. Kawaulize wafanyabishara kama muda wote wanapiga tu maokoto kuna wakati hali si hali.
Kundi hilo juu ni sawa na hili kundi la pili wale ambao wameanza kilimo hawajakutana na soko zuri huenda msimu mmoja au miwili kama walivyotarajia nao hulalamika kilimo hakina tija.
Ukitaka kuona kilimo kinalipa wewe lima tu usikate tamaa huenda wengine wasinielewe hapa namaanisha ukiwa unalima bila kuacha utaona jinsi kilimo kinalipa usiwe mtu wa kujaribu na kuacha.
Niwape mfano rahisi tu: Mwaka jana waliolima vitunguu watanielewa jinsi tumepiga maokoto, gunia 1 limefika hadi 400,000
Msimu wa mwaka juzi wengi hawakuingiza mtonyo kwenye vitunguu bei haikuwa nzuri na mvua ziliwakwamisha waliotegemea kilimo cha mvua hivyo msimu wa mwaka jana hawakulima vitunguu.
Sasa ona yale makundi 2 niliyotaja mwanzo watakavyoingia kwa pupa msimu ujao kwenye kulima vitunguu. Wakikuta bei iko chini kutoka mfano 400,000 kwa gunia mpaka 100,000 kwa sababu wengi wamelima vitunguu wataanza tena kulalamika
Ikiwa kilimo kipo hivyo suluhisho ni nini? Wewe cheza na kauli mbiu ile ile wewe lima tu
Kilimo is not for the weak hasa cha biashara lazima uweke mpunga wa kutosha, usimamizi, tegemea ups and downs