Kilimo si kwa watu dhaifu

Kilimo si kwa watu dhaifu

Sikuwa nime try before so nilikua eager kujaribu msimu huu kwa anticipation ya mvua. Nimejifunza mengi so next time nita boresha zaidi
Kilimo ni experience. Kila msimu unajifunza kitu. Ndiyo maana nikiona hapa JF watu wanavyojadili uzuri wa kilimo kwa kutumia mahesabu na kuja na faida kubwa huwa nawaambia kilimo cha mtandaoni ni tofauti kabisa na hali halisi.
 
Mafanikio kwenye kilimo yapo kwenye stori na calculator; ulikima:
  • Kiangazi kuna gharama mlima za kumwagilia, na ukivuna bei ipo chini kwa kuwa waliovuna ni wengi;
  • Ukilima masika unakutana na wehu wa hali ya hewa (mvua nyingi sana, mvua hafifu sana), na kama ni mahindi ukivuna serikali inafifisha soko makusudi, na wanaibuka wanufaika wa huo uhuni wakitamba kuwa mahindi ni zao la chakula.
  • Ukifanya kilimo unachakaa kinoma, kule tu kushinda shamba juani/mvua, kupigizana kelele na vibarua walevi, kuwaza pasua kichwa ya kupanda kwa pemvejeo, n.k unazeeka fasta. Siku ukikutana na age mate wako wanaeza kukusalimu
 
moja ya malengo yangu makubwa ni kuwa na hekari 100 za kahawa, na 100 za kokoa.....kiufupi kilimo ni biashara na kuanguka, kushuka na kuyumba ni vitu vya kawaida, na kama kilimo kingekuwa rahisi kila mtu basi angekuwa MKULIMA..
Mawazo ya kilimo cha kitajiri.
 
Yako maeneo katika mikoa ya Tanga, Morogoro, Iringa Mbeya, Ruvuma, nk.
Ambayo mvua za masika ni za uhakika.
Kabla ya kulima tafiti kwanza maeneo rafiki kwa kilimo.

Pia Kuna maeneo yenye mito ambayo haikauki.
Pampu za Kichina zipo na zinauzwa Bei rahisi tu.
Kila kazi yenye tija inahitaji tafiti, maandalizi na kufanywa kwa umakini na tahadhari.

Mtu analima hata palizi inamshinda unakuta mazao yapo porini tu.
 
Kilimo sio kamali wazee[emoji4]watu wengi tunalima kwa mihemuko na wala sio kwa mpango WA muda mrefu wengi tunaaminishwa kuwa ukilima umetoka[emoji23]

kutoka popote pale utakapo wekeza muda pesa utapata tuuy sio lazima wote tulime na kama unataka kulima lazima ujue kuwa unaenda kufanya kitu tofauti na shughuli zako so lazima uchukue Muda kujua kilimo na vitu kama hivyo hivyo.
 
Kaka unalima mahindi unasema kilimo sio kwa wanyonge.

Tafuta mahali ulime tumbaku ata heka mbili tuu..
Na usiombe kuwe na mvua nyingi kama msimu huu.
Pamoja na mkopo wa chama cha ushirika ila cash iliyokatika mpaka muda huu ni mil 8. Na hapo bado tumbaku haijachumwa, haijakaushwa, haujagrade, mabelo n.k.
Hapo sijaweka gharama ya kuandaa mabani. Kwa eka 8-9 mabani makubwa ni kuanzia matatu.

Hakuna kilimo kigumu Tanzania hii kama tumbaku.
Lakin nasikia soko lake zuri ?
 
Kaka unalima mahindi unasema kilimo sio kwa wanyonge.

Tafuta mahali ulime tumbaku ata heka mbili tuu..
Na usiombe kuwe na mvua nyingi kama msimu huu.
Pamoja na mkopo wa chama cha ushirika ila cash iliyokatika mpaka muda huu ni mil 8. Na hapo bado tumbaku haijachumwa, haijakaushwa, haujagrade, mabelo n.k.
Hapo sijaweka gharama ya kuandaa mabani. Kwa eka 8-9 mabani makubwa ni kuanzia matatu.

Hakuna kilimo kigumu Tanzania hii kama tumbaku.
Hahaaa hapo bado kudhulumiwa na wale jamaa wa Makampuni ya ununuzi, jamaa wa Bodi ya Tumbaku plus vyama vya Ushirika. Hiko sio.Kilimo, ni utumwa. Nililima.pitia UKONONGO AMCOS kule Inyonga, Mlele Katavi. Hahaaaaaaa pole yako bro, bora ulime bangi tu.
 
Ni kweli
Kwa miaka hii ya usoni soko limetulia sana.
Vijana waliolima eka 2 tu wanatusumbua sana wakirudi mjini.

Chamuhimu utunze vizuri, upate grade ya juu nyingi
Mimi nalima, ila kilimo hiko usijaribu. Ni kilimo unachofanya karibia miezi 8-12 kuanzia kupokea mbegu toka Kampuni sasa inaitwa Mkwawa Leaf kipindi mimi nalima ilikiwa kampuni ya Primium. Uoteshe miche, uanze kupanda, uikuze, ivunwe, uikaushe then uweke kwenye magunia ukauze sokoni(Godown). Ili upate bei nzuri lazima uwahonge wale jamaa wa Kampuni pamoja na Bodi ili wakuwekee daraja za juu lasivyo watakuwekea rejects tu.

Hiyo ni biashara kichaa.
 
Ufugaji nao jau tu[emoji28], unalala na vifaranga 2000 una amka viko 70
Hahaaaaaa, nina mashine ya kutotoreshea vifaranga. Ya mayai 70 tu. Nina uhakika wa vifaranga 60-65 kila.mwezi ila dah, huku kwenye baridi ni kazi sana kufuga. Mara ya mwisho.nilikiwa na vifaranga 130 vya Kuku wa kienyeji, Bata hizi Mallard, Khaki Campbell, Perkins na Bukini. Nimefanikiwa kukuza vifaranga 4 tu vya kuku. Kuna siku nilipiga Ukunga baada ya kukuta vifaranga 30 vimekufa kwa mara 1.
 
Mimi mwezi wa 3 natoa Gobo ekari 15 huku Makete huku nalima Ngano ekari 20. Mwaka huu nina ekari 70 za Mahindi(15 nilipanda mwezi wa 10 mwishoni, 15 nimepanda 5/1/2024), Ngano 20 napanda mwezi 3, Nyanya Chungu 1, njegere nimepanda mwezi wa kwanza mwisho najua nitaivuna wakati wa Pasaka
20240212_185333.jpg
2, Viazi Mviringo 1. Natarajia mwezi wa 4 kupanda tena mahindi ya Gobo huko kwenye kumwagilia 15 acres.
20240216_184142.jpg
 
Mimi mwezi wa 3 natoa Gobo ekari 15 huku Makete huku nalima Ngano ekari 20. Mwaka huu nina ekari 70 za Mahindi(15 nilipanda mwezi wa 10 mwishoni, 15 nimepanda 5/1/2024), Ngano 20 napanda mwezi 3, Nyanya Chungu 1, njegere nimepanda mwezi wa kwanza mwisho najua nitaivuna wakati wa Pasaka View attachment 29083192, Viazi Mviringo 1. Natarajia mwezi wa 4 kupanda tena mahindi ya Gobo huko kwenye kumwagilia 15 acres. View attachment 2908286
Hongera sana kulima kiasi hiki unahitaji kuwa na msuli hasa
 
Kwangu mimi, natarajia kuanza kulima mpunga mwaka huu 24/25 na ndiyo mala yangu ya kwanza kuingia kwenye kilimo.Sijui nitakutana na changamoto gani huko mbeleni.
 
Kilimo Cha mahindi utateseka endapo maandalizi ya mbolea na viuatilifu ni hafifu, mvua kutokuwa za uhakika, kuchelewesha hasa palizi ya kwanza mwisho uchaguzi wa mbegu kulingana na ukanda wa eneo ulilopo.
Wenu mtiifu
Bwana shamba wa mujini
 
Back
Top Bottom