Kilimo si kwa watu dhaifu


Hapa ume maliza kila kitu, hakika hakuna shortcut inahitaji ujiwekeze haswa. Nimefanya msimu huu kama pilot phase lakini nime jitosa haswa haswa nategemea mwakani nisahihishe makosa ya mwaka huu
 
Ukiondoa waalimu,
Hamna watu wanaishi kwa stress nchi hii Kama wakulima[emoji4]
utakua unazungumzia wakulima wa bustani za mchicha huko dar😂😂 hicho sio kilimo ni shughuli za mikono tu kuuchangamsha mwili na kukosa maeneo makubwa , vitendea kazi na mbegu bora zaidi
Kilimo ni moja kati ya kazi nzuri sana ila uwe na passion ! na usiende kulima kwa sababu umehadithiwa na kulimisha kwa simu !! hapo kilimo kitakua Forex ! Kuanguka na kusimama ni sehemu ya kila biashara na kazi
 
Umenena yaliyo kweli mkuu.
Niliwahi lima vitunguu pale Ruaha mbuyuni,nikaweka milion mbili na kitu ila baada ya kuvuna na kuuza nikapata kama laki nne hivi nikaapa sirudii tena na eneo liko tu nimewapa wanakijiji walime bure lisiwe pori.

Nina eneo liko mkuranga,mtoto wa aliyeniuzia akanishawishi sana tulime mahindi hadi nikakubali.Akasema tujaribu na heka chache kwanza.Akasema nipe 1 M nilime heka 4 tu kwanza then tukivuna najua utashawishika tulime hekari zote.Maelezo yake yalininogea,nikashawishika nikampa 1M akasepa.Mwisho wa siku sikupata hata hindi moja la kuchoma.

Nilichojifunza,kilimo kinataka uingie mwenyewe shambani mwanzo mwisho na mimi maisha ya kuishi shamban na manyoka siyawezi.
 
Nakubaliana nawe comradeee nimelima eka 6 za mpunga acha kabisaaa aiseeee
 
Hakuna kitu rahisi,labda kama unafanya ufugaji wa kienyeji wa Bora liende ila ufugaji wa kusaka pesa lazima uone maumivu.
Nimelima na nimefuga, kwaiyo kwangu mimi experience yangu niliyoipata ni bora kufuga kuliko kulima. Unaweza kuuza baaadhi ya mifugo mfano kwangu mimi ni nguruwe ukapata pesa ya kuwalisha wenzake wanaobakia lakini huwezi kukata shamba ukauza baadhi ya mazao ili upate pesa ya mbolea ununue kwa ajili ya yaliyobakia.
 
Ufugaji nao jau tu[emoji28], unalala na vifaranga 2000 una amka viko 70
Dah kuku sijawahi jaribu baada ya kumuona sister broilers wake anabidi awauze siku ya 22 akaja jamaa akachagua wakubwa tupu akaacha wadogo wadogo sister akaanza kuwalisha tena hadi wapate nyama nyama, kuku labda nifuge wa kienyeji wa kula.
 
Wewe kosa lako ushalijua, ulikuwa unataka kulima kwa pdf
 
Nililima maharage ekari 6 mwaka jana zikanikata. Narudia tena mwaka huu. Rungwe.
 
Peasants wanaumiza mgongo, ila farmers wanacheza na mashine tu, tatizo unatakiwa kuqa na mtaji.
Sasa bongo hii wangapi wanamudu mashine, graduates wanaambiwa wakajiajiri kwenye kilimo wanapewa mashine? Mimi ndio maana mambo ya kilomo nilishakataa...kama kulima nitakuwa namsaidia tu mzee tupate chakula ila kwamba niwe siriazi kabisa nitegemee kinitoe kwenye unaskini hapana siwezi kujidanganya, najua jeuri hiyo sina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…