Nimeanza rasmi kilimo cha kuotesha uyoga. Nimegundua kuwa shughuli hizi hazijazoeleka sana na jamii ya watanzania . Natoa wito kwa wakulima wenzangu ambao wangependa kupata maendeleo kupitia kilimo hiki basi tuungane na kuionesha serikali kuwa kilimo cha uyoga kina faida keme kem kuanzia kuwa rafiki wa mazingira, lishe , tiba na uchumi. imeona kuna changamoto kibao ambazo tukiziongea kwa pamoja zitakwisha na hatimaye kuboresha kilimo hiki kwa faida ya jamii. Wenzetu hata wa nchi jirani kama Kenya na Zimbabwe wamepiga hatua kubwa katika kuendeleza kilimo hicho