Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
Kilio cha connection kimekua kikubwa sana huku mtaani kiasi kwamba ishaaminika ndio njia ya uhakika kupata ajira mpaka kupekelea baadhi ya watu ambao wanashikilia vitengo vizuri uko maofisini kuonekana wabaya kwa sababu hawatoi fursa za connection kwa vijana wanaotafuta ajira
Ukweli ni kwamba pamoja na kilio kikubwa cha connection ila wapo watu wengi tu wanaopata connection za kazi lakini hawazitumii vizuri, wanazichukulia poa mwishoe inapelekea kujisahau na kualibu vibarua vyao mpaka kufukuzwa kazi
Mimi nina bro alisaidiwa na sista (sio bro na sister wa tumbo moja ni tunafahamiana tu mtaani) akapata kazi benki, miezi michache baada ya kupata kazi nzuri bro alimwacha mwanamke wake wa muda mrefu aliesota nae nyakati za shida na ashazaa nae mtoto akaoa pisi kali
Ile ndoa haikwenda vizuri migogoro kila siku bro akawa mtu wa pombe sana, baadae akaja kufukuzwa kazi sababu ni ulevi na inasemakana kuna hela alipiga ofisini baada ya hapo pisi kali akamkimbia broo maana alichokifata akipo tena
Maisha yakawa magumu kwa broo na stress kibao akawa mlevi kupindukia akauza gari lake na pesa ikaishia kwenye pombe
Pisi kali akaenda kuolewa na mwanaume mwingine na kipindi anamwacha bro walikua tayari wana mtoto mchanga, mara ya mwisho bro anaonana na mwanae mtoto alikua anamwita broo anko yaan mtoto ajui kama broo ndo baba ake, hata ndugu wa broo wakiomba mtoto aje awajue ndugu zake wa upande wa baba yule pisi kali hataki kabisa.
Mwanamke wake aliezaa nae na akamwacha baada ya maisha kumnyokea alivyosikia ivyo akamsaidia broo wakarudiana akampa hifadhi kwake (huyu mwanamke sio mambo safi ni mchakalikaji wa mishe ndogo ndogo mitaani) ila broo tayari alikua addicted na pombe mpaka ikapelekea kifo chake siku alikunywa pombe kali nyingi sana alafu hajala chochote sukari ikashuka akiwa usingizini kufikia asubuhi akawa tayari ashafariki na uyo ndo mke aliemzika broo.. yule pisi kali hakutokea msibani wala hajawahi kufika kwa ndugu wa broo kutoa pole na taarifa anazo niliona post yake facebook siku broo amefariki.
Katika hali kama iyo unafikiri hata sista atakua na hamu tena ya kumsaidia mtu? Hata uko ofisini kwao akipendekeza jina ofisi ya HR hawezi kumwamini tena maana mtu wa mwisho kumleta alishafanya madudu
Fundisho kwetu job seekers wote ukipata connection ya ajira fanya kazi kwa bidii chunga mienendo yako mtaani, ukifanya vizuri wewe ndani na nje ya ofisi utatengeneza jina zuri kwa job seekers wote ambao bado tupo huku mtaani, ni kweli wapo ambao wanasaidiwa connection na kutengeneza sifa nzuri lakini kama unavyojuwa baya moja linaweza kufunika mazuri yote ila zuri moja haliwezi kufunika mabaya yote, ivyo basi ukipata connection juwa kwamba wewe ni balozi wa sisi ambao bado tupo huku mtaani tunatafuta ajira, tuwakilishe vyema.