Rupia Marko D
Member
- Aug 29, 2022
- 39
- 63
Kilio cha Mnyonge Nchini Tanzania
Kilio cha mnyonge nchini Tanzania ni mada inayogusa nyoyo za wengi, ikihusisha changamoto na matatizo yanayowakumba watu wa kawaida katika jamii. Mnyonge, kwa maana ya mtu mwenye hali duni kiuchumi, kijamii, na kisiasa, anajikuta akikabiliwa na matatizo mengi ambayo mara nyingi hayapati suluhisho la haraka au la kudumu. Makala hii itachambua baadhi ya changamoto kuu zinazowakumba wanyonge nchini Tanzania, pamoja na juhudi na hatua zinazochukuliwa ili kukabiliana nazo.Changamoto za Kiuchumi
Moja ya changamoto kubwa inayomkumba mnyonge ni umasikini. Takwimu za kitaifa zinaonyesha kuwa sehemu kubwa ya Watanzania wanaishi chini ya mstari wa umasikini, wakipata kipato kisichokidhi mahitaji ya msingi kama chakula, malazi, na mavazi. Ukosefu wa ajira na fursa za kiuchumi ni tatizo sugu linalochangia hali hii. Wakulima wadogo wadogo, ambao wanategemea kilimo kama chanzo chao kikuu cha kipato, hukabiliwa na matatizo kama vile uhaba wa pembejeo za kilimo, ukosefu wa masoko ya uhakika, na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri uzalishaji.Changamoto za Kijamii
Kwa upande wa kijamii, mnyonge anakabiliwa na ukosefu wa huduma bora za afya, elimu, na makazi. Huduma za afya ni ghali na mara nyingi hazipatikani vijijini, ambako ndiko kuna idadi kubwa ya watu maskini. Elimu, ambayo ni nyenzo muhimu ya kumkomboa mnyonge, bado ina changamoto nyingi kama vile ukosefu wa vifaa vya kujifunzia, walimu wa kutosha, na mazingira duni ya kujifunzia. Pia, tatizo la nyumba duni na ukosefu wa huduma za msingi kama maji safi na umeme ni mambo yanayoathiri maisha ya wanyonge.Changamoto za Kisiasa
Kilio cha mnyonge hakikosi kugusia masuala ya kisiasa. Mara nyingi wanyonge hawana sauti katika maamuzi yanayowahusu, na wanakosa uwakilishi mzuri katika vyombo vya maamuzi. Hali hii inasababisha kupuuzwa kwa maslahi yao na kutozingatiwa kwa mahitaji yao katika sera na mipango ya maendeleo. Rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma ni mambo mengine yanayochangia kudidimiza maendeleo ya wanyonge.Mnyonge kwa namna moja ama nyingine amekua ni njia ya moja kwa moja ya kukandamizwa na mfumo duni wa kisiasa, siasa ambayo inalenga mlango mmoja, ule mlango ambao unajali zaidi katika kudhoofisha maslahi ya mnyonge,
Msomaji utakua ni muumini wangu wa wazi wa makala hii katika kile ambacho kinaendelea katika nchi ya jirani nchini Kenya ambapo waandamaji wamekuja juu kwenda kinyume na mfumo duni wa siasa wa nchini mwao, ni kwa kile ambacho raia wa kiwango cha chini wanachokidai ni mabadiliko ya wazi katika miswada ya sheria ndani ya nchi, japo hawajachagua Amani wamechagua kushika Fimbo na kuchokona Sharubu za Simba kwa kua kwa muda mrefu walikaa kimya kama swala yule awindwaye na muwindaji na katika hili makala nyingi huandikwa kwa lengo la kumsifu mwindaji, sasa nchini Kenya swala wamejifunza kusoma na kuandika wanataka kuandika nakala ambazo zitamsifu swala na si Muwindaji tena.
Ni namna gani mnyonge anagandamizwa na mfumo duni wa siasa.
1. Kuidhinisha na kupitishwa kwa miswada ambayo haijali maslahi ya mwananchi wa kipato cha chini.
Ndugu msomaji utaungana nami katika hili japo si mwanasiasa mimi, lakini nimekua shuhuda wa wazi kabisa kuona haya yakitokea na kuendelea wazi nchini, kumekuwepo na kusainishwa kwa baadhi ya mikataba na miswada ambayo haijali kabisa maslahi ya mwananchi wa kipato cha chini, na katika mikataba hiyo mingine inaenda mpaka miaka mingi, mkataba unaweza kusainishwa na ukaenda takribani miaka hamsini ijayo, kitendo ambacho kinaviweka hata vizazi vyetu vijavyo katika mlongo mmoja wa kuendelea kutumikishwa na mikataba hiyo. Kitu ambacho sio chema hata kidogo, je kwanini serikali yetu ikubali kusaini mikataba hii ya kikatili
2.Makato ya Kodi.
Hapa ndipo palipo na kisa nao mkasa mkubwa wa kusemewa, ndugu yangu mpendwa msomaji katika hili utaniunga mkonokwa hali ya maisha inayoendelea na jinsi ambavyo serikali yetu kila kukicha, kila panapo itwa leo kumekua na mavumbuzi makubwa sana makato ya kodi, yaani kwa hali inavyoendela itafika kipindi hadi wadada poa ambao wanafanya shughuli za ovyo nao wataanza kukatwa kodi, ni kama kurudi katika kipindi cha ukoloni ambapo watu walikua wanakatwa hadi kodi ya kichwa, kwanini serikali yetu inataka kunyonya kila senti ya mwananchi wa kiwango cha chini?
3. Kudidimizwa kwa sauti ya upinzani bungeni
Japo hili ni matokeo ya awamu ya uongozi wa awamu ya Tano, nchi yetu inakumbwa na siasa duni ikiwa ni matokeo ya wazi ya ukosefu wa sauti ya upinzani, yaani imekua ile ya ndege wanaofanana huruka anga moja,
Je kipi kifanyike? Je mnyonge nae ainuke na kupambania haki yake?
Je aliye kiliyo kisichosikiwa?
MWISHO
Wito wangu wa dhati ni kuwa bado ni mapema kwa mabadiliko ya wazi kufanyika, sitopenda kile kinachoendelea nchini Kenya kijiri nchini Tanzania.
Upvote
4