Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nimekuwa nikifuatilia hoja zinazotolewa Kwenye kikao Cha Bunge kinachoendelea, nilichogundua ni kuwa karibu wabunge wote wanalalamika, kuwa ahadi zinazotolewa na serikali za maendeleo Kwenye majimbo yao hazitekekezwi, au Kwa maneno mengine, wanapigwa changa la macho!
Lakini hebu tutafakari ni kwanini, ahadi hizo za serikali hazitekekezwi.
Kwa utafiti wangu ni kuwa kunatokana na mfumo wetu wa usimamizi mbovu wa matumizi wa hazina ya Taifa.
Waheshimiwa wabunge, wanaona fahari kwao kutangaza Kila kitu, kimefanywa na Rais, bila kujua kuwa kauli zao hizo Zina "negative impact" Kwa kuwa wanampa mwanya wa kutumia hazina ya Taifa atakavyo Rais.
Nitoe mfano, tumekuwa tukisheherekea sana tunaposikia Kwa kauli maarufu ya goli la mama, Kwa timu za Yanga na Simba, Kila zinapofunga magoli Kwenye mechi za kimataifa, wakati inajulikana wazi kuwa huyo Rais hatoi pesa hizo kutoka mifukoni mwake, Bali anazitoa Kwenye hazina ya Taifa, je tumewahi kumuhoji Rais, kuwa anachokifanya ni uvunjifu wa Sheria za fedha??
Ripoti za CAG za Kila mwaka zinaonyesha ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za walipa Kodi wa nchi hii, je tumewahi kuona hatua yoyote inachukuliwa dhidi ya majizi hayo ya pesa zetu za walipa Kodi wa nchi hii??
Kwa hiyo hao waheshimiwa wabunge wetu, naomba mkae kimya Wala msilalamike, hata pale mnaponyimwa pesa za maendeleo Kwenye maeneo yenu, Kwa kuwa nyiye waheshimiwa wabunge, ndiyo mmekuwa mstari wa mbele kutamka Kwa Kila kitu kinachotekelezwa na serikali kuwa amefanya mheshimiwa Rais!😎