A
Anonymous
Guest
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, tunaomba utusikilize sisi wafanyakazi wa Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA) upande wa Tanzania.
Takribani mwaka sasa hatujalipwa baadhi ya stahiki zetu muhimu, ikiwemo mshahara wa mwezi wa nne mwaka 2025, allowance za miezi ya 8, 9 na 10 ya mwaka 2025, pamoja na fedha za likizo ambazo baadhi ya wafanyakazi tunadai kwa takribani miaka mitatu.
Pia, michango yetu ya Public Service Social Security Fund (PSSSF) haijawasilishwa ipasavyo. Hali hii imekuwa ikituathiri sana, hasa tunapokaribia kipindi cha kustaafu.
Wafanyakazi wengi kwa sasa wanashindwa kulipa kodi za nyumba, ada za watoto, gharama za matibabu pamoja na mahitaji mengine muhimu ya familia.
Tumeeleza changamoto hizi mara nyingi kwa viongozi husika, na hata Waziri wa Uchukuzi anafahamu hali hii, lakini bado hatujapata msaada wala ufumbuzi wa kweli.
Mheshimiwa Rais, tunaomba utuangalie kwa jicho la huruma. Tunaendelea kufanya kazi kwa uaminifu na kujituma, lakini maisha yetu pamoja na familia zetu yanaendelea kuumia kila siku.
Tunaomba haki zetu zilipwe na sauti yetu isikike.