A
Anonymous
Guest
Wana-JamiiForums,
Naleta mada hii mbele yenu nikiwa na masikitiko makubwa na dhumuni langu ni kuomba ushauri, lakini pia kufikisha sauti yetu kwa mamlaka husika juu ya ukiukwaji mkubwa wa sheria za kazi na haki za binadamu unaofanywa na Kampuni ya NSK, ambayo inasimamia Hospitali ya Mkoa ya Lumumba hapa Zanzibar.
Mazingira ya kazi yamekuwa magumu na yanashusha morali ya utendaji kazi kwa madaktari na wauguzi kutokana na mambo yafuatayo:
1. Kucheleweshwa kwa Mishahara na Majibu ya Dharau
Mishahara imekuwa ikichelewa kwa muda mrefu bila taarifa yoyote ya dharura au maelezo. Kibaya zaidi, wafanyakazi wanapohoji haki zao, usimamizi unatoa majibu ya dharau kama "The grass is always greener on the other side" na kuwaambia wasiotaka waende TAMISEMI Bara wakalipwe laki 8. Hii ni dharau kubwa kwa taaluma yetu.
2. Udanganyifu wa Mikataba, Mishahara na Makato ya Bima
Kuna mkanganyiko mkubwa wa kimaslahi na ukosefu wa uwazi kati ya madaktari (GPs) na wauguzi. Wakati wa usaili (interview), madaktari waliahidiwa mshahara wa kuanzia (Net/Take-home) wa TZS 1.3 Million, lakini cha ajabu kwenye akaunti zinaingia TZS 1.2M au 1.213M bila maelezo. Zaidi ya hayo, mikataba inaonyesha Gross Salary ni TZS 1.6M yenye makato mbalimbali ikiwemo bima ya afya, lakini cha kusikitisha wafanyakazi hawajawahi kupewa kadi hizo za bima licha ya kukatwa fedha kila mwezi. Vikao vimefanyika lakini hakuna majibu ya kueleweka.
3. Ubaguzi wa Wazi Kati ya Wazawa (Waswahili) na Wageni (Wahindi)
Kuna ubaguzi wa dhahiri wa kimaslahi na vyeo. Wageni (raia wa India) wanapandishwa vyeo bila vigezo vya msingi na wanapokea mishahara mikubwa mno kuliko wazawa wanaofanya kazi kubwa. Mfano, Mhindi anayepita tu usiku kuchukua ripoti analipwa pesa nyingi kuliko Daktari (GP) mzawa aliyepo zamu usiku kucha. Wazawa wakiomba stahiki zao wanaambiwa "You have to earn it." Hivi karibuni wamemteua kiongozi mzawa (MOI) ili tu kuzima kelele na kupoza hali ya hewa (neutralize situation), lakini mfumo wa unyanyasaji uko palepale.
4. Wizi wa Masaa ya Kazi na Unyanyasaji wa Shift (Cheap Labour)
Sheria ya kazi inataka masaa 8 kwa siku (Saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni), lakini kampuni imelazimisha hadi saa 11 jioni kwa kigezo cha kuwa wanatoa lisaa limoja la mapumziko ya chakula cha mchana.
Kutokana na upungufu mkubwa wa Madaktari (GPs), waliopo wanalazimika kufanya kazi kwenye shift za masaa 12 (8:00 AM hadi 8:00 PM). Hapa kuna udanganyifu mwingine; shift ya masaa 12 ilipaswa kuishia saa 1:00 usiku na si saa 2:00 usiku. Zaidi ya hayo, daktari hawezi kuondoka bila kukabidhi shift na kufanya mzunguko (round) mwingine, jambo linalofanya mtu kufanya kazi hadi masaa 14 hadi 16 kwa siku bila malipo ya ziada (overtime).
Tunaomba wadau wa sheria za kazi, Idara ya Kazi Zanzibar, na Wizara ya Afya waingilie kati suala hili. Tunaumia kiakili na kimwili, na jambo hili linaathiri usalama wa wagonjwa tunaowahudumia.
Nawasilisha kwenu kwa ushauri na hatua stahiki.