SoC02 Kilio cha wengi

SoC02 Kilio cha wengi

Stories of Change - 2022 Competition

Pink L

New Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Suala la uchumi hususani ‘pesa’ imekuwa ni kitunguu ambacho kinatumika katika maisha ya kila mtu, kila siku. Usipoitumia ni lazima uiwaze kivyovyote vile. Je, ni nani awezaye kutatua changamoto za fedha? Ungana nami kujua namna inamtoa machozi kila mtu.

KILIO CHA WENGI

Miriam akiwa anatokea chumba cha watoto baada ya kuwalaza aliichukua simu yake iliyokuwa mfukoni baada ya kusikia mlio wa ujumbe “usiwe na mashaka mke wangu mi niko salama” ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa mumewe aliyeitwa Lesso, ambaye alikuwa na mwezi mzima hayupo nyumbani na aliondoka bila kuaga. Miriam baada tu ya kusoma aliipigia ile namba lakini haikupatikana. “mbwa huyu yuko na Malaya wake huko halafu ana…heh we ngoja labda asirudishe tendengu zake hapa” alisonya Miriam kisha akaingia chumbani kwake. Aliichukua picha aliyopiga na mumewe siku ya harusi yao na kuiangalia huku anaifuta futa vumbi.

Machozi yalianza kumtoka kadri alivyoendelea kuiangalia, kamasi nazo ziliungana na machoni na kuulowanisha uso wake “mume wangu mpenzi sijui ni jambazi gani amekuteka ambaye hataki urudi nyumbani anakuruhusu kunitumia ujumbe ila hataki nisikie sauti yako, rudi tu baba mi sina neno mimi ndo kiota chako” aliongea na mumewe pichani mpaka machozi yalipokama. Alipanda kitandani kwake na kufumbata mto aliopenda kuulalia mumewe, hazikupita dakika nyingi usingizi ukamvaa.

Lesso aliyekuwa amejitenga mwenyewe porini kwa ajili ya kazi maalumu aliyopewa na muajiri wake, kwa mashariti ya kutokusema alipo wala kuwasiliana na ndugu zake kwa namba yake aliyotumia bali namba maalumu aliyopewa huku akitakiwa kutuma tu ujumbe na kuizima haraka, alionekana kuwa mtu mwenye mawazo sana. Alizunguka ndani ya chumba kidogo alimokuwamo huku akionekana kufikiria kitu kwa kina. Mawazo yalimmeza kiasi kwamba angeingia mtu na kumshitua basi angeganda kwa mshituko. “pesa, hela, fedha, wewe ni nani? Mbona kila mtu anakutafuta kwa halali na haramu? Ukomo wako ni upi?

Watu, mataifa yote yanalia kwa ajili yako, hata wale wenye uwezo bado hawalali kwa ajili yako, je, mtu anatakiwa awe na wewe kiasi gani ndiyo aseme kuwa ameridhika na wewe?. Hohe hahe pia wanakulilia hata wale walioshika dini wanakuhubiri wewe kwani wewe una nini haswa?” Lesso aliiuliza noti ya shilling mia tano aliyokuwa ameshika mkononi. Aliigeuza nyuma na mbele huku anaaiangalia kwa umakini kabisa.

Akiwa bado anaiangalia moja kati ya simu zake nne zilizokuwa kwenye meza ndogo iliita aliichukua na kusimama “hallo!” Aliongea mara baada ya kuipokea. “ehee niambie bwana Lesso umefikia wapi?” Ilikuwa ni sauti ya mtu aliyempigia simu akimuuliza “mkuu maendeleo si mabaya sana nadhani ndani ya siku mbili nitakuwa nimepata mwanga” alijibu Lesso huku anajikuna kichwa. “sawa tunakutegemea wewe na kama nilivyokwambia, usihofu juu ya familia yako wako salama kabisa na tunahakikisha hawakosi kitu chochote hivyo fanya kazi yako kwa umakini kabisa ili tuwe vinara” aliongea Yule mtu katika simu na kukata mara baada ya kumaliza maongezi yake.

Miriam alishituliwa na hodi ya mtu aliyegonga mlangoni kwake. Alipoangalia saa ilikuwa ishatimu saa mbili na robo asubuhi, alijiinua kiuvivu huku amevalia kanga yake moja na nguo ya kulalia na kuuelekea mlango. Alipofungua alimkuta Devi ambaye alikuja kila siku asubuhi kumletea mahitaji toka siku Lesso atoweke bila kuaga “na leo utanieleza alipo mume wangu” alijisemea Miriam huku anamfungulia mlango.

Siku zote alikuwa akivipokea vitu alivyoletewa na kumuacha kijana nje lakini siku hiyo alimwambia amsaidie kuvipeleka jikoni kwani hakujisikia vizuri. Kijana kwa utii kabisa alibeba mizigo iliyosheheni vyakula mbalimbali, vikiwemo matunda, vyakula na vinywaji vilivyokuwa na lebo ya kampuni aliyofanyia kazi Lesso na kupeleka mahali alipoelekezwa. “mama leo unaumwa kweli maana hujaniuliza yale maswali yako ya kila siku au mzee karudi nini?” Aliongea kijana huku anajichekelesha.

Miriam hakujibu kitu aliguna tuu. Walipofika jikoni Miriam alimuamuru kuweka vyakula ndani ya kabati lililokuwa juu kidogo ya jokofu dogo lililokuwa humo jikoni. Wakati Devi ameinua mikono ili kuweka Miriam alipitisha mikono yake katikati ya makwapa yake na kushika kifua cha Devi. Devi alishituka mpaka mfuko aliokuwa ameushika ukadondoka chini na kusababisha matunda vyakula kuanguka “Ma..” Kijana alijaribu kuongea ila Miriam alimuwahi na kumziba mdomo. Alimlalia mgongoni na kusababisha kifua chake kilichobebelea matiti makubwa kiasi kugusana na mgongo wa Devi huku mikono yake akiipitisha ndani ya shati la Devi na kuanza kumpapasa.

Miriam alimpapasa Devi mpaka akahakikisha amenoga akamuuliza “mume wangu yuko wapi?” Devi kusikia neno mume aliishika mikono ya Miriam kujiondoa lakini Miriam alimzidi ujanja, aliyawahi masikio yake na kuyapuliza taratibu huku mikono akiipitisha kwenye mbavu za Devi na kumfanya asisimke “Lesso yuko wapi? Ukiniambia ukweli nitakupa fedha yoyote unayotaka” Miriam alimuuliza tena huku anamg’atang’ata masikio yake “yuko porini kuna kazi maalumu amepewa, ambayo inahitaji utulivu wa hali ya juu huwa nampelekea tuu chakula na kurudi ila ni siri haitakiwi ajulikane alipo” Devi alijikuta akitoboa siri ambayo alihimizwa na muajiri wake kutokuitoa.

Miriam kusikia hivyo alifurahi sana alimpiga Devi busu la shavuni na kumshukuru, aliitoa mikono yake mwilini mwa Devi “kwa hiyo unaniachaje sasa?” Devi aliuliza huku macho yakiwa mekundu “sijakuacha tutaendelea siku nyingine mume wangu akitoweka?” Alijibu Miriama huku anatabasamu, tena akiwa hatua kadhaa mbele kuelekea chumbani kwa watoto wake kuwaamsha ili wajiendae kuelekea twisheni kwani walikuwa likizo. Alimwambia Devi akitoka aurudishie mlango wa nje. Devi alitoka huku anajipigapiga kichwa na kujisonya.

Siku ambayo Lesso alitakiwa kuwasilisha kazi aliyopewa iliwadia. Katika chumba cha mikutano walijaa wafanyabiashara mbalimbali na wamiliki wengi wa kampuni. Viongozi wa serikali wa nchi mbalimbali hasa wale waliokuwa wakihusika na sekta ya uchumi walikuwepo pia. Lesso aliteuliwa na kampuni yake kuandaa majibu ya namna ya kutatua tatizo la uchumi lililoonekana kuwa changamoto ulimwenguni kote.

Sababu pekee iliyopelekea yeye kuteuliwa ni uadilifu wake kazini na upendo aliokuwa nao juu ya kazi yake aliyoifanya, kwani sifa zake zilienea sehemu nyingi na kufanya kampuni nyingi kumtolea macho. Ulipofika muda way eye kuzungumza kila mtu alikaa kimya kumsikiliza “tatizo la uchumi ni la kila mtu na kila nchi ulimwenguni na ndiyo maana hata mataifa yaliyoendelea bado yanatafuta pesa, hakuna mtu au nchi ambayo ishafika hatua ya kusema kuwa uchumi wetu ni imara, tuna fedha za kutosha hivyo hatuhitaji kutafuta tena.

Ni wajibu wa kila nchi na kila kampuni kusimamia rasimali zake yenyewe na kutokurasmisha kwa yeyote awaye. Kila nchi ijitengenezee uchumi wake lakini waruhusu uwekezaji ambao utabadilishana nguvu kazi na pesa au bidhaa na pesa, au teknolojia na pesa, kufanya hivyo itasaidia kila nchi kujiiinua kichumi. Lakini mpaka dunia inafika ukomo hakuna nchi itakayoridhika na uchumi wake” lesso alimaliza kuongea na mvua ya makofi ilishindilia mawasilisho yake.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom