GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kutokana na asili / nature ya Kazi zao Makondakta wengi nchini wamelalamikiwa sana na Wake / Wapenzi wao hasa kutokana na Vitendo vyao wa kila siku usiku wakilala tu huwa wanawahi Kuota Ndoto zao nyingi huwa ni za kupiga Kelele kama wanaita abiria na kupiga bati la Daladala hali ambayo mara nyingi wahanga wa Kero hizi / Mateso haya huwa ni wao.
Mwanamke mmoja ambaye Mume wake ni Kondakta hapa jijini Dar es Salaam amesema kwamba kiukweli imefikia muda hadi hivi sasa anatamani tu Mume wake achelewe kurudi au apate tu Nyumba ndogo kwani kiukweli huwa akirudi basi huwa anakosa sana amani hasa akijua kuwa baadae wakati wa Kulala kuna zoezi lingine la mateso ambalo linamsubiri.
" Huu sasa ni mwaka wa 13 Mume wangu ni Kondakta lakini kwa jinsi anavyonikera wakati tukiwa tumelala na akiota kiukweli nimechoka. Yaani hadi Wapangaji wenzangu wamechoka kwani kila siku usiku wakati kumetulia kabisa tumelala utamsikia anaota na akisema kwa nguvu kabisa Mbagala kupitia Chang'ombe kisha utamwona anaanza kunipiga Mimi vibao kama vile anaruhusu Gari / Basi kuondoka kisha anashtuka na kuniomba radhi ", alisema Mke huyo ambaye jina lake linahifadhiwa ili asije kupishana na Talaka ya Mumewe kama akijulikana.
Humu JF naamini kabisa kuwa kuna Wataalam wa Kutukuka kabisa wa Saikolojia hivyo kama hawatajali basi tunawaomba waje na watupe ufafanuzi pamoja na suluhisho la kudumu la hii tabia ya Makondakta wengi wa Madaladala kwani kiukweli hii tabia imekuwa ni Kero mno kwa Wanawake wengi nchini wenye Waume Makondakta.
Nawasilisha.