Kilio hiki cha Wake za Makondakta wa Daladala nchini nani atakisikiliza ili wapewe msaada?

Kilio hiki cha Wake za Makondakta wa Daladala nchini nani atakisikiliza ili wapewe msaada?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kutokana na asili / nature ya Kazi zao Makondakta wengi nchini wamelalamikiwa sana na Wake / Wapenzi wao hasa kutokana na Vitendo vyao wa kila siku usiku wakilala tu huwa wanawahi Kuota Ndoto zao nyingi huwa ni za kupiga Kelele kama wanaita abiria na kupiga bati la Daladala hali ambayo mara nyingi wahanga wa Kero hizi / Mateso haya huwa ni wao.

Mwanamke mmoja ambaye Mume wake ni Kondakta hapa jijini Dar es Salaam amesema kwamba kiukweli imefikia muda hadi hivi sasa anatamani tu Mume wake achelewe kurudi au apate tu Nyumba ndogo kwani kiukweli huwa akirudi basi huwa anakosa sana amani hasa akijua kuwa baadae wakati wa Kulala kuna zoezi lingine la mateso ambalo linamsubiri.

" Huu sasa ni mwaka wa 13 Mume wangu ni Kondakta lakini kwa jinsi anavyonikera wakati tukiwa tumelala na akiota kiukweli nimechoka. Yaani hadi Wapangaji wenzangu wamechoka kwani kila siku usiku wakati kumetulia kabisa tumelala utamsikia anaota na akisema kwa nguvu kabisa Mbagala kupitia Chang'ombe kisha utamwona anaanza kunipiga Mimi vibao kama vile anaruhusu Gari / Basi kuondoka kisha anashtuka na kuniomba radhi ", alisema Mke huyo ambaye jina lake linahifadhiwa ili asije kupishana na Talaka ya Mumewe kama akijulikana.

Humu JF naamini kabisa kuwa kuna Wataalam wa Kutukuka kabisa wa Saikolojia hivyo kama hawatajali basi tunawaomba waje na watupe ufafanuzi pamoja na suluhisho la kudumu la hii tabia ya Makondakta wengi wa Madaladala kwani kiukweli hii tabia imekuwa ni Kero mno kwa Wanawake wengi nchini wenye Waume Makondakta.

Nawasilisha.
 
Ili kusudi tusonge mbele maana maendeleo hayana chama ( In Baba J voice). Nimesema makonda chapeni kazi ,achaneni na habari za ndoto

Sent From Kisana Kiki Iphone
 
Ninaomba kuwa research assistant katika hili swala
 
Wangejirekodi kwenye sipika kama wamachinga wafanyavyo, Wakawa wanaweka betri kisha wanaifungulia sipika hiyo na kuanza kuita abiria.
 
We Nawe Stor Zako Ckuhz Za Ktoto Toto! Inamaana Waalimu Nao Wanaota Wanafundisha? Wachungaj Wanaota Wanahubiri? Watangazaj Redioni Je? Wanaofanya Kaz Za Kupga Makelele Wapo Wengi Na Inategemea Na Mtu Mwenyewe Alivyo, Hata Km Ni Mchezaj Mpira Km Ni Mtu Wa kuota Usiku, Bac Ataota Anaomba Apewe Pasi. So Hii Haipo Kwa Makondakta Tu, Ni Mtu Yeyote Mwenye Tatizo Hlo Hata Km Anampenz Nje Ya Ndoa, Ucku Anaweza Kuropoka Mazungumzo Yao.
 
Hahaha jf nouma kwa kweli
 
Hii ndio hoja ya Kimakinikia kabisa
[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Hii hadithi ni nzuri sana inakihusu chama cha mapinduzi, wananchi ndiyo wake na CCM ni makondakta. Asante mkuu
 
Serikali iweke ukomo wa utumishi ktk sekta ya ukondakta... Miaka 13 konda? Angekuwa serious angeshakuwa Dere kitambo sana....@jokes
 
Back
Top Bottom