Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Nadhani wengi wetu wameshatazama teaser za filamu zinazokuja Badlands pamoja na Killer of Killers. Teasers mbili ambazo ndo zinaendeleza filamu za Predators, viumbe ambavyo vinajulikana kitaalamu kama Yautja. Wakati Badlands ikiwa ni filamu huku Killer of Killers ikiwa ni Animation.
Killer of Killers ni animation filamu ambayo inaonekana itakuwa nzuri sana kwani imekusanya matukio ya vipindi vitatu tofauti, WAKATI WA VIKINGS, WAKATI WA ENDO JAPAN PAMOJA NA WAKATI WA VITA VYA PILI VYA DUNIA. Teaser yake pekee imeonesha kuwa filamu itakuwa nzuri sana, imeleta imani kuwa itarudisha ule ubora wa Yautja ambao ulikosekana kwenye Filamu ya Prey, mambo ya usawa yasituharibie filamu za Predator.
Ukiachana na Killer of Killers pia imetoka teaser ya Predator: Badlands ambayo imepokewa kwa mwitikio hasi, huku watu wakionesha wasiwasi kuwa itakuwa ni filamu mbaya.
Wanaodai hili wanaonesha kuwa kiuhalisia Yautja sio viumbe vya kuviua kizembe kama yule wa kwenye filamu ya Prey, shughuli ambayo Dutch na Dillon walikutana nayo sio shughuli nyepesi, wanajeshi walioneshwa vita bomba.
Yautja ambao amehusika kwenye filamu ya Predator (1987) anabaki kuwa ndio Yautja bora kutokea, kazi safi kabsa kutoka kwa John McTiernan lakini pia kwa uchache wake tumeona uwezo wa Yautja katika filamu za Predator 2 (1990), Predators (2010), pamoja na Predator (2018) na sasa tutegemee **Yautja mwingine bora wa kwenye Killer of Killers**
Yautja wa kwenye filamu ya Prey (2022) ni kituko cha millenia hata kama utetezi ni kuwa ilikuwa ni kabla ya teknolojia ila historia za hawa viumbe Yautja teknolojia yao ipo mbali sama, tangu miaka milioni na zaidi.
Na huyu Yautja ambaye anaonekana yupo kwenye Predator: Killer of Killers (2025) shughuli yake sio ya kitoto, ni sawa na Yautja ambaye alikuwa kwenye The Predator (2018) yule Yautja ambaye ni Upgraded Predator mjomba mwenye urefu wa mita 3.35, kuna kipande, Upgraded Predator alimkamata Predator mwingine kama anakamata panzi.
Chuma Killer of Killers itakuwa sokoni Ijumaa ya Juni 6 huku Badlands ikitarajiwa kutoka Ijumaa ya Novemba 7.
TEASER YA KILLER OF KILLERS HII HAPA
TEASER YA PREDATOR: BADLANDS HII HAPA
CHUKUA MUDA NA TAZAMA HIZI TEASER MBILI JE TEASER IPI KWAKO IMEKUWEKA MKAO WA KUSUBIRI KUONA SHUGHULI ZA YAUTJA DUNIA KWA MARA NYINGINE?