Nadhani wengi wetu wameshatazama teaser za filamu zinazokuja
Badlands pamoja na
Killer of Killers. Teasers mbili ambazo ndo zinaendeleza filamu za Predators, viumbe ambavyo vinajulikana kitaalamu kama
Yautja. Wakati
Badlands ikiwa ni filamu huku
Killer of Killers ikiwa ni Animation.
Killer of Killers ni animation filamu ambayo inaonekana itakuwa nzuri sana kwani imekusanya matukio ya vipindi vitatu tofauti,
WAKATI WA VIKINGS, WAKATI WA ENDO JAPAN PAMOJA NA WAKATI WA VITA VYA PILI VYA DUNIA. Teaser yake pekee imeonesha kuwa filamu itakuwa nzuri sana, imeleta imani kuwa itarudisha ule ubora wa
Yautja ambao ulikosekana kwenye Filamu ya
Prey, mambo ya usawa yasituharibie filamu za Predator.
Ukiachana na
Killer of Killers pia imetoka teaser ya
Predator: Badlands ambayo imepokewa kwa mwitikio hasi, huku watu wakionesha wasiwasi kuwa itakuwa ni filamu mbaya.
Wanaodai hili wanaonesha kuwa kiuhalisia
Yautja sio viumbe vya kuviua kizembe kama yule wa kwenye filamu ya
Prey, shughuli ambayo
Dutch na
Dillon walikutana nayo sio shughuli nyepesi, wanajeshi walioneshwa vita bomba.
Yautja ambao amehusika kwenye filamu ya
Predator (1987) anabaki kuwa ndio
Yautja bora kutokea, kazi safi kabsa kutoka kwa
John McTiernan lakini pia kwa uchache wake tumeona uwezo wa
Yautja katika filamu za Predator 2 (1990), Predators (2010), pamoja na
Predator (2018) na sasa tutegemee **Yautja mwingine bora wa kwenye
Killer of Killers**
Yautja wa kwenye filamu ya Prey (2022) ni kituko cha millenia hata kama utetezi ni kuwa ilikuwa ni kabla ya teknolojia ila historia za hawa viumbe
Yautja teknolojia yao ipo mbali sama, tangu miaka milioni na zaidi.
Na huyu
Yautja ambaye anaonekana yupo kwenye
Predator: Killer of Killers (2025) shughuli yake sio ya kitoto, ni sawa na
Yautja ambaye alikuwa kwenye
The Predator (2018) yule
Yautja ambaye ni
Upgraded Predator mjomba mwenye urefu wa mita 3.35, kuna kipande,
Upgraded Predator alimkamata
Predator mwingine kama anakamata panzi.
Chuma
Killer of Killers itakuwa sokoni Ijumaa ya Juni 6 huku
Badlands ikitarajiwa kutoka Ijumaa ya Novemba 7.
TEASER YA KILLER OF KILLERS HII HAPA
TEASER YA PREDATOR: BADLANDS HII HAPA
CHUKUA MUDA NA TAZAMA HIZI TEASER MBILI JE TEASER IPI KWAKO IMEKUWEKA MKAO WA KUSUBIRI KUONA SHUGHULI ZA YAUTJA DUNIA KWA MARA NYINGINE?