Jeshi la polisi wilayani Kilolo, mkoani Iringa linamshikilia mwenyekiti wa Kijiji cha Mtandika kwa mahojiano zaidi kuhusu tuhuma za kuchukua fedha kwa wafugaji na kusababisha migogoro kati ya kundi hilo na wakulima, huku watu wengine wanaohusika na kugawa ardhi kinyume cha utaratibu nao wakisakwa.
Makunga amekamatwa baada ya mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Kituo cha polisi Wilaya ya Kilolo ambao ulilenga kupata suluhu kwenye kadhia hiyo.