Uchaguzi 2020 Kilombero Ubunge tunakwenda na Asenga, Lijualikali tupa kule

Uchaguzi 2020 Kilombero Ubunge tunakwenda na Asenga, Lijualikali tupa kule

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nimeshangazwa sana na huu msimamo wa wana Kilombero kwamba ubunge wanakwenda na Aboubakary Asenga na kwamba Lijualikali arudie kazi yake ya kupanga vitabu Kanisani.

Wandamba kweli makauzu pamoja na kazi kubwa anayoifanya Lijualikali ya kumbomoa Mbowe lakini bado hamumwelewi?

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hao Wana Kilombero hawajui wenye mamlaka ya kuchagua Mbunge mwaka huu Ni kamati za CCM, ambazo zinapewa maagizo na Magufuli
 
johnthebaptist,
Hivi kweli wana Kilombero mliokuwa tayari mmekwamuka kutoka CCM mnataka kurudia matapishi? Nijuavyo Assenga ni CCM labda kama atakuwa CHADEMA siku hizi.

Watu wa Ifakara mlionesha weledi mkubwa kwa kuachana na CCM. Naunga mkono sana Lijua apigwe chini vibaya tena kwa adhabu kali manake ametuaibisha mno.
 
Hao Wana Kilombero hawajui wenye mamlaka ya kuchagua Mbunge mwaka huu Ni kamati za CCM, ambazo zinapewa maagizo na Magufuli
Mtifuano ni Mkubwa Safari hii wanaccm wanamtaka mtu mwenyekiti nae anataka watu wake wakuja kubadili katiba ndio wapite,patamu hapo mwenyekiti anamiliki polisi wananchi wanamiliki kura,kumkomoa mwenyekiti ni lzm watasapoti upinzani,chama chakavu Mali ya familia ni lazima kisambaratike mwaka huu
 
Huyo Lijuakali alikuwa Katia nia Momba kwa Silinde kwa mujibu wa John Mrema.
 
Mtifuano ni Mkubwa Safari hii wanaccm wanamtaka mtu mwenyekiti nae anataka watu wake wakuja kubadili katiba ndio wapite,patamu hapo mwenyekiti anamiliki polisi wananchi wanamiliki kura,kumkomoa mwenyekiti ni lzm watasapoti upinzani,chama chakavu Mali ya familia ni lazima kisambaratike mwaka huu
Piga ua huko lazima CCM abebe hata wakipigia kura upinzani wanapoteza muda tu
 
Kama Ni mwana CCM poa tu,,shida yetu Ni CHADEMA kupotolea mbali huko!!! Lijualikali atapata kazi nyingine.
 
Hatumchagui chasaka huku bora aende huko kwao akagombee, vyasaka ni wabaguzi sana wana ukabila kama Kenya walivyo. Yani huwezi kuta Engineer Wa kisumu anafanya kazi Mombasa. Kila MTU na kwao ndo wanayopenda.hukumbuki Mbowe alikuja na wazo la majimbo kujitegemea ,kila Hela ya Mwanza iendeleze Mza na sio ikaendeleze mtwara
 
Kwa yale mapambio Lijuakali hawezi kukosa kazi,si ajabu akaja kuwa mkuu wako wa wilaya,save my comment.
 
Hongera wandamba...dawa ya hawa watu ndiyo hiyo. Kama yule mwanapunda aliyembeba Yesu wakati anaingia Yerusalem, baada ya Yesu kusurubiwa akaona aaaa akarudi peke yake ili apate mapokezi yale yale pale yaliyomkuta ni aibu.

Ndiyo hawa vijana wadogo tamaa mbele
 
Back
Top Bottom