Kilomita za Gari

Wakuu Gari ikiwa imetembea kilomita ngapi haifai kununua......
Msaada tafadhali
Inategemeana na ukubwa engine mfano gari za cc isiyozidi 1900 husinunue ikiwa imezidi 60000 km

Cc isiyozidi 3000 chukua gari chini ya 150,000km

Cc isiyozidi 5200 unaweza ukachukua gari chini ya 300,000 km..
 
Inategemeana na ukubwa engine mfano gari za cc isiyozidi 1900 husinunue ikiwa imezidi 60000 km

Cc isiyozidi 3000 chukua gari chini ya 150,000km

Cc isiyozidi 5200 unaweza ukachukua gari chini ya 300,000 km..
Unaweza kutoa sababu ya huu ufafanuzi wako?!

Hivi unajua gari ukinunua unapewa warranty km 100,000 au miaka 3 yaani kinachotangulia?
Kuna gari 60,000km ni sawa na mchezaji amemaliza warm up sasa ndio anaingia uwanjani kucheza mechi.

Mimi sasa hivi nina gari ya cc2000 imetembea 235,000 km iko vizuri kuna watu wananiambia kila siku nikijisikia kuiuza niwaambie kwasababu wanajua ilivyo na ninavyoitunza.
 
Km sio tu inaonesha uchakavu wa mashine, kuna vitu vingi kama vile vya body parts. Pia ukongwe wa engine sio sababu ya kupunguwa pulling power, mkuu, unaweza ukakuta gari ina 50,000 Km lakini ikawa haina nguvu kama same engine yenye 150,000 km. Hapa cha kuzingatia ni Maintainance ya engine yako. Sometimes engine ilofanyiwa overhaul hutokea kuwa na more power than engine ambayo haijafanyiwa overhaul.

Muhimu mtu kama unataka kununa gari KM sio kigezo kizuri, What if engine imebadilishwa imewekwa nyengine? Unaweza ukareplace same engine without the ECU ukatumia ile ya zamani, na ukitumia ya zamani km hazibadiliki kisa umetia new engine, itaread pale pale pa zamani tu. Wewe tafuta fundi mzuri aisikilize engine inaliaje, mana mara unakuta engine unasikia milio ya knock na engine yenyewe ndo kwanza ina 30,000km. Test the car, drive it to its limit, fikisha karibia redline kwenye rpm, itizame vipi itarespond.

Mimi binafsi nikitaka kununua gari lazima niipe extreme tests. Ni muhimu kujua gari kama inarespond vilivyo wakati unadrive kwenye different conditions.
 
Ukipata gari ya Mjeruman(BENZ,VW na BMW) nyingi zina speed 220kph hadi 300.Hapo Land Cruiser VX-V8 atasubiri. Uzuri wa Mjerumani gari zake zina high speed na ni nzito sana hivyo kuwa na balance kubwa iwapo barabarani.
Ubaya wa mjerumani are built to fail. Reviews nyingi sana mbaya kwenye haya magari, kiluxury hayana mpinzani, ki reliability? Mjapani kashindikana. Afu hawa wajeru kitu kidogo lakini kina complication hatari, wanaita german engineering wenyewe, ovyo kabisa. yaani gari zao zikiwa out of warrant bora uza faster, mana kwanzi hapo utaona ukitia pesa mfukoni inapotea, utasema chuma ulete kumbe jini benz na bimmer 😀
 
nilitaka anzisha uzi huu juz juz nkawa nakosa muda....

msaada wenu

me naona gari nzuri iwe haijafika km 100,000 itakuwa haisumbui

mitandaoni kuna gari za ajabu

eti gari ya 2002 ina km 50,000 tu

nahisi wanazichezea

ila kwa wateja wa daihatsu boon/ passo hako ka gari si cha kununua wakat kamevuka 100,000km
 
Hata km1 tu haifai maana imetumika tayari vyema upate 0 km ingawa kwa inchi yetu ni vigumu kupata
 
Pamoja na service km 300000 ndio standard, isizidi hapo
 
Kuna kitu ambacho waswahili wengi hawajui,gari nyingi za bongo km zinarudishwa nyumba ina laki na n nusu mtu anaiweka elfu sitini.Gari ikiuzwa toka Dubai au Ulaya na Japan wewe chukua tu kwa sababu watakupa full details za gari.
 
me sa hivi naangalia muda tu yani gari ya mwaka 2005 to date sio mbaya
 
Aina gani hyo gari yako mkuu?.
 
Du nilizaliwa nikakuta baba ana gari hadi sasa ni miaka 36bado anaiendesha nahisi hadi azeeke ataniridhisha ina maana gari haina ukomo wa km waweza nunua any km unayokuta nayo gari

Inategemea anatumia lini.

Baba anakaa upanga mtaa wa Olympio anasali kanisa la TAG -Ccc pale mzumbe dar campus.
Anaendesha kim 1 kwenda na kurudi .

Kazini ni posta na anachukuliwa na gari ya ofis.hapo je
 
Usinunue garikwaku angalia kilomita ztakupoteza kwani kunautala sikuizi wakuludisha kilomita nyuma nazkasoma gari imekimbia kilomita chache sana baada yahapo matatizo yakaanza.


Na hasa timing belt. Hii hukatika inapofika wastani wa 100,000km hivyo wakirudisha nyuma ni hatari sana. Maana ikikatika inaweza sababisha kuuwa vitu vingine vingi.
 
Ki talaamu ukiona gari mfano

Subaru legacy ya mwaka 2005 ina kilomita 50000

Afu ukaona ingine hyo hyo subaru ya mwaka 2010 ina kilomita 150000

Basi hyo yenye kilomita 150000 ndio bora coz gari kiwa ya miaka ya nyuma afu ina kilomita chache maana yake haliendeshwi sana na pia inamanisha ka inaendeshwa basi ni city driving so mashine haipati moto ipasavyp automatic uchakavu mkubwa...

Pendelea kuchagua magari ya miaka ya karibun yenye kilomita nyingi kuliko ya zaman yenye kilomita chache....
 
Japo sina gari lakini nimejifunza jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…