CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kilosa Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka leo akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, amefanya kikao kazi na viongozi wa Jeshi la Polisi.
Viongozi hao wa Jeshi la Polisi waliongozwa na ACP Hassan Maya, Afisa Mnadhimu wa Polisi, Mkoa Morogoro, Mkuu wa Polisi Wilaya Kilosa pamoja na askari wa vyeo mbali mbali ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mkakati kusimamia utekelezaji wa masuala ya Ulinzi na Usalama Wilayani humo katika kuelekea Kilosa yenye fursa kwa wote.
#Kilosaye2Fursaze2
#Uongoziwapamoja
#MaendeleoEndelevu