- Source #1
- View Source #1
Wakuu,
Nimeona video huko Facebook upepo mkali unabeba viti na inadaiwa kuwa imetokeo huko Kilwa kwneye moja ya mkutano wa wagombea ubunge katika mchakato wa kuomba kura za maoni kwa wajumbe huko CCM
Nimeona video huko Facebook upepo mkali unabeba viti na inadaiwa kuwa imetokeo huko Kilwa kwneye moja ya mkutano wa wagombea ubunge katika mchakato wa kuomba kura za maoni kwa wajumbe huko CCM
- Tunachokijua
- Madai
Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebookkwa nyakati tofauti walichapisha kipande cha video katika kurasa zao za mitandao ya kijamii wakiambatanisha na ujumbe unaoshiria kuwa tukio linaloonekana kwenye video hiyo linahusiana na mchakato wa uchaguzi wa wanaowania nafsi ya kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya ubunge.
Kipande hiko cha video kinaonehsa upepo mkali ukisoma baadhi ya viti vilivyokuwa kwenye uwanja ikishiria vilikuwa vimepangwa kwa ajili ya mkutano. Mtumiaji mmoja aliandika kuwa;
“NDUNBA NANGAI HUKO KILWA Mgombea ubunge atumiwa onyo kali la kimbunga
Chautawanya mkutano wake kwa jeuri kubwa, wajumbe meza kuu wasukwa sukwa kama karatasi.
wananchi waapa kutousogelea mkutano wake.”
Na mtumiaji mwingine yeye alindika kuwa;
Wale waliokatwa wameanza "michakato" rasmi. Acha nchi ichangamshwe maana Oktoba mbali
Uhalisia wa Taarifa hiyo
Baada ya ufuatiliaji wa kina, JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo haina uhusiano na mchakato unaoendelea ndani ya CCM.
JamiiCheck imebaini kuwa kipande hiko cha video hakijarekodiwa nchini Tanzania bali kilirekodiwa nchini Kenya na kuchapishwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuanzia Agosti 1, 2018 katika mtandao wa You tube.
Video hiyo ni la tukio lilitokea eneo la Ukambani nchini Kenya wananchi walipokuwa kwenye moja wa Injili. Vyanzo kutoka nchini Kenya viliripoti kuwa mara baada ya tukio hilo la kushangaza kutokea eneo hilo waumini waliokuwepo walikimbia mbali na eneo hilo.
“Video ya kisulisuli kilichovuruga maandalizi ya mkutano wa injili huko Ukambani, Kenya imesambaa sana mitandaoni.” - Gazeti la Punch liliripoti
“Waumini walibaki na mshangao mkubwa baada ya kisulisuli kutokea ghafla na kufagia kila kitu kilichokuwa njiani wakati wa mkutano wa injili huko Ukambani, Kenya.
Wale waliokusanyika kwenye mkutano huo wa injili walianza kukimbia hovyo mara walipoona upepo ukivuma kwa nguvu na kupeperusha viti pamoja na spika hewani.” - Adom online iliripoti Agosti 2, 2018. Vyanzo vingine vilivyoripoti ni Wiseloaed