The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wananchi wa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wamepongeza Serikali kupitia Wakala wa barabara nchini Tanroads Mkoa wa Lindi kwa kuanza kazi ya urejeshaji wa miundombinu ya kudumu ya barabara na madaraja ambayo yameathiriwa wakati wa mvua za Elnino na Kimbunga Hidaya.
Wakizungumza wakati wa ziara ya Meneja wa wakala huo Mkoa wa Lindi ya kukagua kazi zinazoendelea,baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nanjilinji A na B,Mwajuma Majota na Shafii Kirupe wamesema wanashukuru kwa ujenzi unaoendelea Kwani wakati wa mvua wanashindwa kwenda kufanya shughuli zao za kijamii kutokana na Mto Nakiu na Kigombo ambayo imekuwa ikitumika kama njia ya mkato ya kuwafikisha kwenye mashamba yao na kuifikia pia Wilaya ya jirani ya Ruangwa kujaa maji na kukatisha mawasiliano.
Meneja wa Tanroads Lindi Mhandisi Emily Zengo anasema barabara ya Kiranje ranje-Nanjilinji-Namichiga hadi Ruangwa pamoja na daraja la Mbwemkuru tatu ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa na mvua za Elnino na Kimbunga Hidaya na serikali imetafuta fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 20.55.
Fedha hizo tayari zimetolewa kwa awamu hii kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Kigombo lenye urefu wa mita 25 pamoja na makaravati saidizi mawili huku mto Nakiu daraja lenye urefu wa mita 70 linajengwa na kwamba hadi kufikia disemba 2025 madaraja yote yanayojengwa katika barabara hiyo yatakuwa yamekamilika.
Kukamilika kwa ujenzi wa madaraja hayo kunatajwa kuwa kutawasaidia wananchi wa maeneo hayo ambao wengi wao ni wakulima wa ufuta kuusafirisha na kuyafikia masoko Wilayani Kilwa na upande wa Ruangwa na kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii kama afya kwa urahisi.