Kim Philby: Jasusi wa MI6 aliyesaliti kila mtu mpaka kivuli chake mwenyewe

Kim Philby: Jasusi wa MI6 aliyesaliti kila mtu mpaka kivuli chake mwenyewe

Kile kinachofanya kisa cha huyu mwingereza Philby kuwa cha kutisha zaidi si kwamba hakuiba Taarifa za siri pekee, bali pia kwa miaka mingi alikuwa mmoja wa watu muhimu waliotegemewa zaidi ndani ya mfumo aliokuwa anausaliti .. 💀💀☠️
Nakubari nakubari mcTobby shusha vitu
 
3


Usaliti aluoufanya Kim Philby haukuwa tu kushindwa kwa mtu mmoja. Ni kwamba Ulitikisa misingi ya mashirika ya ujasusi ya Uingereza, hasa MI5 na MI6, kwa miongo kadhaa baadaye. Hizi ndizo athari mbaya zaidi zilizoachwa na Philby.

1. Kupoteza uaminifu kati ya MI5 na MI6
Kabla ya Philby kufichuliwa, MI5 na MI6 zilifanya kazi kwa karibu kama ilivyo CIA na FBI pale marekani.
Baada ya kashfa hii ya usaliti wa Philby, mashirika haya yakawa yanatupiana lawama.MI5 iliilaumu MI6 kwa kushindwa kumchunguza Philby ipasavyo.
MI6 nayo iliona MI5 imekuwa na mashaka kupita kiasi na inataka kumsulubisha Kim kama kuikomoa MI6.
Mvutano ulikuwa mkubwa wa ndani ya haya mashirika kuhusu nani aliyefanya kosa na nani anapaswa kuwajibika.Kwa mara ya kwanza, mashirika hayo mawili yalianza kuhoji uwezo wa kila mmoja kulinda siri za taifa. Na hadi Leo hii mashirika haya yamekuwa na bifu la ndani kwa ndani ingawaje ni mashirika ndugu kabisa .

2. Athari nyingine ni kwamba Marekani ilianza kutokuiamini Uingereza kwenye maswala mazima yanayohusisha Siri za Taifa.Athari kubwa zaidi ilikuwa katika uhusiano wa Uingereza na Marekani.
Mashirika ya Marekani kama yaani CIA na FBI yalikuwa yanajua kuwa afisa wa juu wa MI6 alikuwa agent wa Soviet kwa miongo mingi.
Swali lilikuwa:
"Kama Philby aliweza kufika juu kiasi hiki ndani ya MI6, ni nani mwingine bado yupo?" Sasa hapo Marekani ilianza kuishirikisha , baadhi ya taarifa nyeti kwa tahadhari zaidi na Uingereza. Ile Hali ya kuaminiana baina ya mashirika haya kulipotea.

3. Maaget wengi walikamatwa au kuuawa

Hii ndiyo athari ya moja kwa moja na ya kusikitisha zaidi.Kwa miaka mingi Philby aliwapa Soviet Majina ya maagent,Operesheni za siri.
Njia za mawasiliano n.k.Matokeo yake ni kwamba
Mitandao ya mawakala ilivunjwa,Operesheni zilifeli,Watu walikamatwa naBaadhi yao waliuawa.
Hata leo, idadi kamili ya waathirika wake haijulikani.

4. Alipelekea Mageuzi makubwa ya ukaguzi wa usalama katika kuajiri maafisa wa MI5 na MI6.

Kabla ya Philby, mfumo wa Uingereza ulitegemea sana:
Asili ya familia aliyotoka ,Elimu ya shule za kifahari,Mapendekezo ya marafiki n.k. lakini Philby alikuwa:Mwanafunzi wa Cambridge.
Mtu wa aliyetokea kwenye familia ya upper class na Mwenye marafiki wenye ushawishi...
Kwa vigezo Hivyo alionekana "hawezi kuwa msaliti."..💀💀☠️😀
Baada ya kashfa yake, MI5 na MI6 zilianza:
Uchunguzi wa kina wa historia za wafanyakazi wake.
Ukaguzi wa mara kwa mara wa usalama.
Kufuatilia uhusiano wa kisiasa na itikadi za wafanyakazi ili kuepukana na aibu na madhara hapo baadaye kama aliyosababisha Philby.
Kanuni ya zamani ya "mwungwana wa Kiingereza hawezi kuwa msaliti" ilikufa rasmi.

5. Kuvunjika kwa hadhi ya MI6
Kwa muda mrefu MI6 ilikuwa imejivunia kuwa moja ya mashirika bora duniani.Lakini ilipobainika kuwa Philby:Aliingia ndani ya mfumo,Akapanda hadi nafasi za juu,Akadumu kwa zaidi ya miaka 30 bila kugunduliwa Hadhi ya MI6 ilipata pigo kubwa sana.
Wanahistoria wengi huona kashfa ya Philby kama moja ya aibu kubwa zaidi katika historia ya MI6.

6. Kuzaliwa kwa "utamaduni wa mashaka"
Athari ya muda mrefu ilikuwa ya kisaikolojia.
Baada ya Philby:
Kila afisa aliyekuwa na tabia ya ajabu alishukiwa.
Kila operesheni iliyofeli ilionekana huenda imevujishwa.
Kila uvumi kuhusu "mole" (jasusi wa ndani) ulianza kuchukuliwa kwa uzito.
MI5 na MI6 ziliingia kipindi cha mashaka makubwa kuhusu uwezekano wa kuwa na wasaliti wengine.

7. Kufichuliwa kwa Cambridge Five
Usaliti wa Philby ulisaidia kufichua kwa kiwango kikubwa mtandao wa Cambridge Five.

Kufikia miaka iliyofuata, ilibainika kwamba watu wengine kama:
Guy Burgess
Donald Maclean
Anthony Blunt
John Cairncross
walikuwa pia wanafanyq kazi na Soviet.
Hii ilionyesha kwamba tatizo halikuwa mtu mmoja pekee, bali mtandao mzima uliokuwa umejipenyeza katika taasisi za serikali.

Anyway licha ya Philby kuwa shujaa kwa Soviet, hakuweza kuinusuru anguko la umoja wa USSR.
Kim Philby alifia Moscow mwaka 1988 na kuzikwa kwa heshima ya Hali ya juu na maafisa wa KGB akiwa na umri wa miaka 76.


Over........
 
Huyo Philby hakuwa na familia (mke na watoto)?
Sijagusia upande wa familia yake.. ila alikufa akiwa ameoa mara tatu... Mkewe wa pili aliyeitwa Aileen Philby alikuwa na Changamoto ya afya ya akili... Alikuwa anaugua ugonjwa fulani hivi wa kiakili wa kujidhuru peke yake ili kupata Attention ya mmewe (nimesahau jina).. maana me wake alikuwa bize sana na kuuza Siri za Taifa kwa wanywa Vodka wa Russia.. huyu Aileen alikufa kwa mshtuko wa moyo kutokana na kuzidisha pombe KABLA ya Philby kutorokea Russia.😎
 
Back
Top Bottom