Kim & The Boys afariki dunia

Invisible

JF Admin
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,286
Reaction score
8,380
Promota maarufu Kim & The Boys amefariki jioni ya leo mida ya saa 9 (kwa masaa ya Tanzania).

Jina lake ni Joakim lakini la kiislam alipewa AbdulHakim akijulikana zaidi kwa majina ya "Kim & The Boys"

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa mwenzetu Mkandara ambaye yupo Dar.

Poleni wafiwa.
 
Mkuu wa kaya samahani ndio nani na alikuwa ana promote nini?? nimejaribu kua google vinakuja vitu tofauti kbs.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.
 
R.I.P Kim&The Boyz a.k.a DJ Kim mzee wa Yo Rap Bonanza
 
Mkuu wa kaya samahani ndio nani na alikuwa ana promote nini?? nimejaribu kua google vinakuja vitu tofauti kbs.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.

Ni Abdul Akim Magomelo..Alikuwa DJ na Promota maarufu wa Muziki na Mashindano ya Disko enzi za ujana za akina Masanilo..Pia alikuwa ni mmojawapo wa viongozi wakuu wa TDMA enzi hizo
 
Mwenyezi Mungu amlaze Mahali pema peponi "Abdul"
Amen!
 
Huyu jamaa ni so instrumental, so instrumental, so instrumental katika maendeleo ya muziki wa kizazi kipya na bongoflava Tanzania.

Najua kuna eighties babies na wengine wasiomjua wanaweza kuuliza huyu ni nani? Huyu pengine anajulikana sana kama aliyewapandisha stejini kwenye mashindano ya "Yo Rap Bonanza" Kina Saleh Jabri, Kwanza Unit, Hard Blasterz, Dar Young Mob (Enzi hizo wako na 2 Proud) hata kina No Name, Ras Pompidou, GWM (Wazee wa Temeke, enzi hizo hakuna Kibra wala Gangwe Mobb) etc.

Hii ilikuwa kabla ya videos za muziki wa vijana hawa katika televisheni ya ITV, early nineties, kabla hata ya enzi za Professor Jay (Professor Jay - Initially "Nigger Jay, until bestowed the professorship by John Dillinger Matlou -alikuwa mshika bendera wa Hard Blasterz tu, enzi hiyo ikiwa Terry na Willy)

Sikumbuki fujo wala disorderly conduct hata moja kwenye concerts zake, kuanzia Empire / Empress Cinema mpaka Avalon, mpaka Jumba la Wakorea ukisikia concert la Kim unajua magwiji wote wanaenda kukutana, inakuwa kama conference fulani hivi.

Kim alikuwa mtu fulani so social lazima niseme, alikuwa karibu na watu, alikuwa anajichanganya na watu wa rika na socio-economic standing zote vizuri, kuanzia machizi wangu wa Temeke kina GWM mpaka watoto wa Oysterbay kina marehemu Rob, kuanzia watoto wanaojaribu kuingia kwenye fani mpaka wazee wazima kina Ras T, alikuwa anajichanganya vizuri sana.

Medani ya muziki Tanzania imeondokwa na pioneer mmoja aliyeanzisha kitu ambacho mpaka leo tunajivunia.

Jamaa alitengeneza vibes kali, aliunganisha vijana wa Dar - na Tanzania in some ways- kwa kupitia muziki tukajiona wote wamoja bila kujali umetoka wapi.I should know, I was there.

Najisikia vibaya kwamba niko mbali na siwezi kuhudhuria mazishi yake.
 
it is so sad kumpoteza huyu jamaa,blueray ameeleza yote tunayohitaji kusema
R.I.P KIM
INNA LILLAH WA INNA ILLAIHI RAJ'UUN
 
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu DJ Kim Pema Peponi.
 
Another fallen hero, and a few young bros cant even understand who the hell is Kim; hii ni another justification kwamba hatutunzi kumbukumbu zetu kwa hawa pioneers kwa culture, social na tz history in one way on another

Enzi za Yo rap bonanza nikiwa tambaza, ulikuwa ni wakti wa kuazima hadi viatu kwenda kuosha kwenye shoo

REST IN PEACE MKUU AND I AM PRAYING WILL DO MORE TO TREASURE THESE FALLEN STARS
 
Huyo asijekuwa na dini katoa maelezo marefu sana... R.I.P Kim
 

you said it all mpwa...nami kama wewe nasikitika nipo mbali nashindwa kwenda kumzika Kim!!sioni udhuru unaoweza kuvunjika ungefanya nisiende kumzika huyu ndugu,pioneership yake peke yake kwa mziki wa nyumbani tunaouskiliza na kuuangalia sana kipindi hiki ingenilazimisha,achilia mbali ile personal relationship nilikuwa nayo naye...
inna lilahi wa inna illahi rajuun...tupo njia moja...
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Amen!
 
Nimesikitika sana hasa majonzi yangu yapo pamoja na wafiwa.
Mungu awafariji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…