Huyu jamaa ni so instrumental, so instrumental, so instrumental katika maendeleo ya muziki wa kizazi kipya na bongoflava Tanzania.
Najua kuna eighties babies na wengine wasiomjua wanaweza kuuliza huyu ni nani? Huyu pengine anajulikana sana kama aliyewapandisha stejini kwenye mashindano ya "Yo Rap Bonanza" Kina Saleh Jabri, Kwanza Unit, Hard Blasterz, Dar Young Mob (Enzi hizo wako na 2 Proud) hata kina No Name, Ras Pompidou, GWM (Wazee wa Temeke, enzi hizo hakuna Kibra wala Gangwe Mobb) etc.
Hii ilikuwa kabla ya videos za muziki wa vijana hawa katika televisheni ya ITV, early nineties, kabla hata ya enzi za Professor Jay (Professor Jay - Initially "Nigger Jay, until bestowed the professorship by John Dillinger Matlou -alikuwa mshika bendera wa Hard Blasterz tu, enzi hiyo ikiwa Terry na Willy)
Sikumbuki fujo wala disorderly conduct hata moja kwenye concerts zake, kuanzia Empire / Empress Cinema mpaka Avalon, mpaka Jumba la Wakorea ukisikia concert la Kim unajua magwiji wote wanaenda kukutana, inakuwa kama conference fulani hivi.
Kim alikuwa mtu fulani so social lazima niseme, alikuwa karibu na watu, alikuwa anajichanganya na watu wa rika na socio-economic standing zote vizuri, kuanzia machizi wangu wa Temeke kina GWM mpaka watoto wa Oysterbay kina marehemu Rob, kuanzia watoto wanaojaribu kuingia kwenye fani mpaka wazee wazima kina Ras T, alikuwa anajichanganya vizuri sana.
Medani ya muziki Tanzania imeondokwa na pioneer mmoja aliyeanzisha kitu ambacho mpaka leo tunajivunia.
Jamaa alitengeneza vibes kali, aliunganisha vijana wa Dar - na Tanzania in some ways- kwa kupitia muziki tukajiona wote wamoja bila kujali umetoka wapi.I should know, I was there.
Najisikia vibaya kwamba niko mbali na siwezi kuhudhuria mazishi yake.