Kimaro hana lolote kwa jimbo lake. Mashamba anataka yagawiwe watanzania wenye uwezo wakati wale wasio na uwezo hawana hata ardhi ya kulima mahindi na maharagwe. For sure watu wenye uwezo ni pamoja na yeye, naamini anatamani sana yale mashamba. Kimaro ni bepari, hata anapokuwa anasemea habari za mafisadi ni kwa vile hakupata chance naye angekuwa ni mmoja wao. Mzee huyu anajulikana kwa unafiki wake.
Ndesamburo ndiye aliyeweka wazi katika swali lake la nyongeza kuwa anataka mashamba yagawiwe wale wote wako katika abject poverty. Ambapo ni sahihi kabisa ukilinganisha na uhaba wa ardhi kwa watu wa Kilimanjaro, hasa wachagga.
Yale mashamba kwa sasa yanalima mbogamboga na si kahawa na wengine wanalima mahindi, tofauti na mikataba ilivyoelekeza. Mengine hayalimwi kabisa. Nafahamu kuwa ardhi ni mali ya serikali, lakini ikumbukwe kuwa ardhi ile iko mkoani Kilimanjaro na wana haki nayo. Ni afadhali wananchi wa maeneo husika wagawiwe na walime mazao maana kahawa imeshaonekana ni failure kabisa.
Serikali jalini maslahi ya wananchi kwanza, na nina hakika hata meneo yaliko mashamba hayo hata ukigawa hawatoshelezi kwani demand ni kubwa mno. I wish ningekuwa President wa nchi hii. Ningefanya maamuzi ya ajabu yote yakimlenga mzalendo. Yaani tumesahau wazalendo hawa ambao ndiyo wanawapa kura?? Too sad.