Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 530
- 1,446
Majuzi bhana, nikaenda kuangalia salio. Kuna kipindi niliweka Tsh 100,000 kwenye akaunti yangu ya CRDB nione kama kuna hela ya kutoa ili nisaidie jambo fulani. Nilichokutana nacho huwezi amini 🙌🙌— nadaiwa kama Tsh 56,547.68 na hela yangu yote imekula! 😂 Nikaamua kuwaachia kadi yao na deni lao, watajua wenyewe wanalifanyaje.
Niliweka akiba, bado haitoshi, halafu mnanidai tena! Laki moja yangu haikutosha kabisa 😥.
Haya mabenki, kama huna hela, usijipeleke Bank. Bora uende kafanye mishe zako. Kama una dili la muda na akaunti ya benki, basi tumia kwa muda huo. Ukimaliza, rudisha kadi ndani. Haya mabenki yana makato ya kinyonyaji sana. Ukiangalia mikodi na makato yao kwenye taarifa zao ni uhuni wa hali ya juu kabisa.
Sasa hivi, ukiweka hela wanakata, ukitoa hela wanakata, ukiomba kadi mpya wanakata, kuona salio wanakata, na hata kuomba Bank statement wanakata.
Hakuna unafuu wala usalama wa hela zako benki. Ukijua una hela kule, umepigwa. Benki imebaki kwa wafanyabiashara na watumishi wa serikali maana wao hata wakikatwa hawaumii—hela zinaingia na kutoka. Lakini mimi kwa sasa, kuweka hela benki sitaki. Bora nibaki na M-Pesa 😆—hata kama kuweka ni bure, siku nataka kutoa ndipo naumia kwenye makato.
Hizi benki tuwaachie wenye nazo waendelee kuzijivunia 😆. Sisemi usitumie benki hapana, kila mmoja ana mtazamo wake. Huenda kesho nikijiweza, nikawa mteja mzuri wao 😆. Ila kwa sasa, ngoja nizisake hela zangu. Nilizonazo nazipenda, sitaki ziliwe tena! 🤣