Huku Rwanda, Kagame usiku anawasha vogue lake(tena anaendesha mwenyewe) anazunguka mitaa ya Kigali.Ole wake meya akute kadhia ka hii ya Dar-es- Salaam,kesho yake mtu hana kazi. Mtamuita dikteta au vyovyote mtakavyo lakini watu wanjua bwana mkubwa hataki upuuzi.
Matatizo hapo matatizo ni matatu:
1)Wanaotakiwa kusimamia kampuni zinazo zoa uchafu ndo hao hao wenye kampuni hizo.
2)Ukikuta ni kampuni ya mtu ambae kapata kazi kwa njia ya halali utakuta bei aliyoweka kufanya hiyo kazi ni 10% less of the budgeted price. Ngoma inakuwa inogile pale budgeted price inapokuwa ndogo ukilinganisha na ukubwa wa kazi.Hapo utakuwa ubabaishaji kwa kwenda mbele na kitu kidogo kitafanya kazi.
3)Mwisho kabisa ni tabia za wana bandari salama.
Kigali ukifika siku ya kwanza kwa jinsi mji unavyongaa utadhani huko Europe,ukweli ni mzuri japokuwa unauma. WANABANDARI SALAMA NI WACHAFU,TUNATEMA MATE HOVYO,TUNATUPA TAKATAKA HOVYO,TUNAJISAIDIA HOVYO KILA KITU ...............HOVYO HOVYO. Baadae tunamlaumu Kimbisa au Lukuvi, Wafanye nini?
KUANZIA LEO UKIONA MTU ANATENGENEZA UCHAFU , kamata peleka polisi na kisha mpigie simu Lukuvi uone ka mji autapendeza. NIWAJIBU WETU KULIPENDA JIJI NA VIONGOZI WETU ITABIDI WATENDE KWA KUONA AIBU.
TUWACHE KULALAMIKA NA KUPENDA KUFANYIWA KILA KITU.