Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Zaidi ya watu 179 wamefariki dunia nchini Vietnam kufuatia maporomoko ya ardhi na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Yagi.
Habari kutoka Vietnam zinasema watu wengine zaidi ya 140 hawajulikani walipo kufuatia janga hilo, na juhudi za kuwatafuta zinaendelea.
Kimbunga Yagi kinaelezwa kuwa ndio kibaya zaidi kuwahi kupiga Kaskazini mwa Vietnam katika kipindi cha miaka 30.
Kimbunga hicho kwa siku ya Jumamosi kilisababisha upepo mkali na mvua kubwa ambapo pia kilipiga katika maeneo kadhaa ya Ufilipino na China na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo na miundombinu.
Shirika la umeme linaloendeshwa na Serikali ya Vietnam, EVN, siku ya Jumatano limelazimika kukata umeme kwa baadhi ya maeneo yaliyofurika maji kwenye mji mkuu kutokana na wasiwasi wa usalama.
Hata hivyo, baadhi ya shule huko Hanoi zimewaambia wanafunzi wabaki nyumbani kwa wiki nzima, wakati maelfu ya wakazi wa maeneo ya tambarare wamehamishwa.