MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 65
- 81
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ameendelea kuweka rekodi katika Jimbo la Vunjo ya kufanikisha kuanza kwa ujenzi wa daraja linalounganisha vitongoji vya Msufini na Kisimani kata ya Makuyuni hali itakayowarahisisha mawasiliano ya wananchi toka upande mmoja kwenda mwingine katika kufuata huduma, usafirishaji wa mazao, vifaa vya ujenzi pamoja na kuvutia wakazi wapya katika maeneo hayo. Mradi huo unagharimu shilingi milioni 423 na unatarajiwa kukamilika Novemba 20, 2024.
Dkt Kimei anasema anamshukuru Mungu sana kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan kwani katika kipindi cha miaka takribani minne Jimbo la Vunjo limepata takribani shilingi bilioni 41 katika miradi ya maendeleo ambayo ni rekodi haijapata kutokea hapo kabla. Akitoa mifano amesema
Mpaka mwaka 2020 Vunjo ilikuwa na zahanati 13 tu za serikali. 2021 mpaka leo wamefanikiwa kupata fedha za kujenga zahanati mpya 12 na kufanya zahanati kuwa 25 na zote zimepata wataalam, dawa na vifaa tiba hivyo wananchi wanapata huduma karibu zaidi na gharama nafuu.
2. Mpaka mwaka 2020 Vunjo ilikuwa na vitongoji 155 tu kati ya 346 ndio vilivyofikiwa na umeme. 2021 mpaka leo wameongeza vitongoji 153 na kufanya jumla ya vitongoji 308 kati ya 346 kuwa vimefikiwa na umeme.
3. Mpaka mwaka 2020 Vunjo ilikuwa na vituo vya afya viwili vya Mwika Msae na Kirua Vunjo ambavyo vilijengwa kabla ya uhuru na kituo cha wagonjwa wa Nje (OPD) Himo. 2021 mpaka leo Vunjo imepata vituo vipya vya afya vitatu Marangu Hedikota (kimekamilika na kinatoa huduma, bado kazi za mwisho kwenye jengo la mama na mtoto), Kahe (kimekamilika na kinatoa huduma), Koresa (kipo mbioni kuanza ujenzi) na kituo cha wagonjwa wa Nje (OPD) Himo kimepandishwa hadhi kuwa kituo kamili cha afya (kimepata mashine ya matibabu ya meno, gari la wagon, ultrasound, digital x-ray, vitanda vya wagonjwa na wajawazito kujifungua pamoja na wataalam mbalimbali wa afya)
Soma Pia: Kimei aweka rekodi nyingine kwa kufanikisha mradi wa ukamilishaji daraja la Sembeti - Samanga
Ndio maana wanasema awamu hii Dkt Kimei anaweka rekodi juu ya rekodi